SHUJAA WA SIMBA; ABdallah Juma akionyesha jezi namba yake kwa mashabiki baada ya kufunga bao |
Na Prince Akbar
MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC leo ni kama wamekata
tiketi ya kuingia Robo Fainali Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la
Kagame, baada ya kuichapa Ports ya Djibouti mabao 3-0 Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Shujaa wa Simba leo, alikuwa mshambuliaji mpya kutoka Ruvu
Shooting ya Pwani, Abdallah Juma aliyeingia kuchukua nafasi ya Amri Kiemba mwanzoni
mwa kipindi cha pili aliyefunga mabao mawili dakika za 60 na 73 na Felix Mumba
Sunzu Jr. aliyefunga moja kwa penalti dakika ya 64
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika bila nyavu za
Ports kutikisika, na katika kipindi hicho Sunzu, mshambuliaji wa kimataifa wa
Zambia, alipoteza nafasi tatu za wazi mno, za kufunga mabao akiwa amebaki yeye
na kipa, Kalid Ali Moursal.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mserbia, Milovan Cirkovick
kipindi cha pili kuwaingiza Juma Nyosso kuchukua nafasi ya Haruna Shamte, Abdallah
Juma aliyechukua nafasi ya Kiemba na baadaye Uhuru Suleiman kuchukua nafasi ya
Haruna Moshi ‘Boban’ yaliisaidia Simba.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi tatu baada ya
kucheza mechi mbili na sasa inashika nafasi ya tatu kwenye Kundi A, nyuma ya
URA yenye pointi sita na AS Vita yenye pointi tatu na wastani mzuri wa mabao. Simba
itamaliza na AS Vita ya DRC, mechi ambayo itakuwa kali kwa sababu timu zote zina
pointi sawa.
Simba SC; Juma Kaseja, Haruna Shamte/Juma Nyosso, Amir Maftah,
Shomary Kapombe, Haruna Moshi ‘Boban’/Uhuru Suleiman, Mussa Mudde, Felix Sunzu,
Amri Kiemba/Abdallah Juma, Mwinyi Kazimoto, Lino Masombo na Kanu Mbivayanga.
Porst FC; Kalid Ali Moursal, Kadar Abass Abanel, Mohamed Omar
Arab, Abdourahman Isman, Jean Paul Niyobabariba, Mehdi Ahmaed Moumin, Vincent Taboko Agbor,
Omar Mohamed Hassan/ Ryad Said Awad., Daher Hassan Ali, Roland Ayuk Agbor
na Gasama Jean Bosco/ Abdillahi Hamadou.
katika mchezo uliotangulia wa kundi hilo, URA ya Uganda, ilikuwa
timu ya kwanza kufuzu Robo Fainali ya baada ya kuichapa mabao 3-1, AS Vita ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
Mabao ya URA yaliwekwa kimiani na Sula Bagala mawili na
Robert Ssentongo, wakati la kufutia machozi la Vita, inayofundishwa na kocha w
zamani wa Yanga, Raul Jean Pierre Shungu lilifungwa na Mutombo Kazadi.
Mwinti Kazimoto kazini |
MSIMAMO WA KUNDI A
P W D L GF GA GD Pts
URA 2 2 - - 5 1 4 6
AS Vita 2 1 - 1 8 3 5 3
Simba 2 1 - 1 3 2 1 3
Ports 2 - - 2 - 7 -7 -
Kapombe anapasua |
Sunzu anafunga penalti |
Abdallah Juma anakwenda kufunga |
Mashabiki wa Simba kwa raha zao |
0 comments:
Post a Comment