SHUJAA; Patrick Kanu Mbivayanga mfungaji wa bao pekee |
Na Prince Akbar
BAO pekee la kiungo wa
kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Patrick Kanu Mbivayanga,
usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar limetosha kuipeleka Simba SC,
fainali ya Kombe la Urafiki.
Kanu, aliyeletwa kwa mabingwa
hao wa Ligi Kuu na Mkongo mwenzake, marehemu Patrick Muteesa Mafisango, alifunga
bao hilo dakika ya 57, akiunganisha krosi ya mshambuliaji wa kimataifa wa
Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr., aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya
Salim Kinje.
Hadi mapumziko, hakuna timu
iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na kipindi cha pili baada ya kocha
Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick kufanya mabadiliko, ndipo ushindi
ukawezekana.
Dakika ya 85, Sabri Ramadhan ‘China’wa
All Stars, alikwamisha mpira nyavuni, lakini refa akasema alikuwa ameotea.
Kwa matokeo hayo, Simba
itacheza na Azam FC katika fainali keshokutwa, Uwanja huo huo wa Amaan.
Katika mchezo huo, kikosi cha
Simba kilikuwa; Juma Kaseja, Shomary Kapombe, Amir Maftah, Lino Masombo/Juma Nyosso,
Obadia Mungusa, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Mussa Mudde, Abdallah Juma/Jonas
Mkude, Kanu Mbivayanga/Haruna Moshi ‘Boban’ na Salim Kinje/Felix Sunzu.
Katika mchezo uliotangulia
mapema jioni, mabao mawili ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Herman
Tcheche, yalitosha kuivusha Azam FC hadi fainali ya michuano hiyo, baada ya
kuwafunga mabingwa wa Zanzibar, Super Falcon 2-0 kwenye Uwanja huo huo wa
Amaan, Zanzibar.
Tcheche alifunga bao la kwanza
dakika ya 67, akiunganisha krosi ya Hamisi Mcha wakati bao la pili, alifunga
kwa penalti, dakika ya 77, baada ya Samir Haji Nuhu kuangushwa kwenye eneo kla
hatari na Samir Said dakika ya 77.
Katika mechi hiyo, Azam ilipata
pigo dakika ya 54, baada ya mshambuliaji wake Gaudence Exavery Mwakimba
kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 54 kwa kumpiga kiwiko Abdul Ally.
0 comments:
Post a Comment