Na Prince Akbar
KLABU ya Simba imewataka wapenzi na mashabiki wake kuendelea
kujiunga na huduma ya kutuma ujumbe mfupi kupitia huduma ya Fan Simba Club ili
kupata taarifa mbalimbali za Simba ikiwemo matokeo ya michuano ya kombe la
Kagame inayoanza Julai 14 mwaka huu na masuala
ya Usajili.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Klabu hiyo
Ezekiel Kamwaga alisema kupitia huduma hiyo mashabiki wa Simba watapokea
taarifa za kila siku ambazo wao watakuwa wa kwanza kuzipata
kupitia huduma hiyo.
Alisema pia itaisaidia klabu ya Simba kujiongezea mapato
yatakayoiwezesha klabu hiyo kuendesha mambo yake katika ufanisi mkubwa ikiwa ni
pamoja na kusajili wachezaji wazuri.
Kwa upande wake Meneja
Kampeni wa Kampuni ya Push Mobile Talib Rashid ambao wameingia mkataba
na klabu ya Simba kupitia huduma ya sms Fan Simba Club wamefunga droo ya bahati
nasibu waliokuwa wakiichezesha kwa klabu ya Simba kupitia huduma hiyo kwa kutoa
pikipiki na bajaji.
Bahati nasibu hiyo iliyokuwa ikichezwa kwa kipindi cha miezi
mitatu sasa imefungwa kwa kuwapata washindi ambao ni wanafunzi wa shule za
Sekondari huku mmoja akiwa ni Tito Zakaria kutoka shule ya Sekondari ya
Mong'ola iliyopo Dodoma aliyejishindia pikipiki na Mohamed Ibrahim kutoka shule
ya Sekondari ya Chandama iliyopo Kondoa na kujishindia bajaji.
0 comments:
Post a Comment