Sunzu kushoto na Kapombe kulia wakimpongeza Boban |
Mudde akimpongeza Boban |
Na Prince Akbar
SIMBA imetoka sare ya 1-1 na AS Vita ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), katika mchezo
wa mwisho wa Kundi A, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, Felix Sunzu alikosa penalti dakika ya
kwanza ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida, kufuatia beki
mmoja wa Vita kuunawa mpira kwenye eneo la hatari, lakini shuti lake lilipanguliwa
na kipa Mcameroon, Lukong Nelson kabla ya mabeki wake ‘kuosha’.
Hadi mapumziko, Vita walikuwa mbele kwa bao 1-0, lilifungwa
kwa penalti na Etikiama Taddy, dakika ya 35, baada ya Juma Said Nyosso kuunawa
mpira kwenye eneo la hatari.
Simba ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Haruna Moshi ‘Boban’
aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Patrick Kanu Mbivayanya dakika
ya 66.
Katika mchezo huo, Simba ilipata pigo dakika ya 27, baada ya
mshambuliaji wake Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’ kuumia kifundo cha mguu na
kutoka nje, nafasi yake ikichukuliwa na Kiggi Makassy.
Kwa matokeo hayo, Simba imemaliza kama mshindi wa tatu katika
Kundi A na itamemnyana na Azam katika Robo Fainali Jumanne, wakati mabingwa watetezi
Yanga watamenyana na Mafunzo Jumatatu.
Robo Fainali nyingine zitakuwa kati ya URA na APR na Atletico
dhidi ya Vita.
Simba SC; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Shomary Kapombe, Lino
Masombo, Juma Nyosso, Mussa Mudde/Salim Kinje, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Felix
Sunzu, Abdallah Juma na Kanu Mbivayanga/Haruna Moshi.
AS Vita; Lukong Nelson, Ilo ngo Ilifo, Issama Mpeko, Ebunga Simbi,
Mutombo Kazadi, Lema Mabidi, Etekiama Taddy, Mapuya Lema, Magola Mapanda,
Basilua Makola, Mfongang Alfred.
KIggi anatia krosi |
Kipa wa Vita akiruka bila mafanikio kuokoa shuti la Boban lililotinga nyavuni |
RATIBA ROBO FAINALI
Julai 23, 2012
Mafunzo vs Yanga
URA vs APR
Julai 24, 2012
Atletico vs AS Vita
Azam vs Simba SC
0 comments:
Post a Comment