Mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania,
Mbwana Ally Samatta ‘Sama Goal’ (pichani), leo anatarajiwa kuiongoza klabu yake, Tout
Puissant Mazembe mjini Lubumbashi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika
dhidi ya Berekum Chelsea ya Ghana, kuanzia saa10:30 jioni. Mechi nyingine ya
Kundi lao, itakuwa ni kati ya wapinzani wa jadi katika soka ya Misri, Zamalek
na Al Ahly, kuanzia saa 5:00 usiku. Mbwana, au Poppa kama wamuitavyo nyumbani
Mbagala, aliiambia BIN ZUBEIRY juzi kwa simu kutoka Lubumbashi, kwamba yuko fiti
na anaamini ataanza- akaomba Watanzania wamuombee dua aendelee kung’ara Afrika.
Katika mechi ya kwanza ugenini dhidi ya Ahly, Samatta aliifungia bao Mazembe. |
0 comments:
Post a Comment