Samatta. Picha ta Maktaba |
Mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally
Samatta ‘Sama Goal’, leo ametoa pasi zote za mabao mawili ya klabu yake, Tout Puissant Mazembe,
kwenye Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa
Afrika dhidi ya Berekum Chelsea ya Ghana, uliomalizika hivi punde kwa sare ya
2-2.
Mapande yote ya Samatta leo yalitumiwa vema na Tressor Mputu
Mabi katika dakika za 11 na 32 kuipatia mabao Mazembe, wakati Chelsea ya Ghana
ilionyesha yenyewe ni moto kweli kwa kupata sare Lubumbashi. Mabao ya Chelsea
yalifungwa na Emmanuel Atukwei Clottey katika dakika za 71 na 84. Dakika ya 75,
Samatta alimpisha Francis Kasonde wakati huo wenyeji wakiwa wanangoza 2-1,
lakini kutoka kwake kulisababisha jahazi kuzama kabisa.
Katika mchezo wa kwanza, Mazembe ilifungwa 1-0 wiki
iliyopita, Samatta akifunga bao la kufutia machozi Cairo na sasa mabingwa hao
mara nne Afrika wana pointi moja tu ndani ya mechi mbili, kuashiria kwamba wana
kibarua kizito kutimiza ndoto zao za kutwaa ndoo ya tano Afrika.
Mechi nyingine ya Kundi lao, itafuatia saa 5:00 usiku, kati
ya wapinzani wa jadi katika soka ya Misri, Zamalek na Al Ahly.
0 comments:
Post a Comment