Samatta akiwa n a jezi ya Taifa Stars |
MBWANA Ally Samatta, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania,
usiku huu ameifungia bao moja Tout Puissant Mazembe ya DRC, ikilala 2-1 mbele
ya wenyeji Al Ahly katika mchezo wa Kundi B wa Ligi ya mabingwa Afrika,
uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Jeshi, mjini al-Qahirah, Cairo, Misri.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC, alifunga bao hilo
dakika ya 85, akiunganisha pasi ya Kasusula, ikiwa ni dakika 20 tu tangu
aingie uwanjani akitokea benchi kwenda kuchukua nafasi ya Lungu.
Mabao ya wenyeji yalifungwa na Emad Moteab dakika ya 12,
pasi ya Waleed Soliman na Gedo dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya
kutimu dakika 90 za kawaida za mechi hiyo, akiunganisha pasi ya Sayed Moawad.
Katika mechi hiyo ya kwanza kwa TP Mazembe katika kundi hilo, mchezaji wake wa Kimwaki alipewa kadi nyekundu dakika ya 81 baada ya kumchezea rafu Mohamed Aboutrika.
0 comments:
Post a Comment