HISPANIA jana waliifunga Italia 4-0 katika fainali ya Euro 2012 na watu wanasema ni kipigo kikali, lakini mbele ya Ruvuma ni cha mtoto tu.
Ruvuma imethibitisha kuwa mwiba mkali katika michuano ya Copa
Coca-Cola mwaka huu baada ya leo asubuhi (Julai 2 mwaka huu) kuishushia
Lindi kipigo cha mabao 7-2.
Hadi
mapumziko kwenye mechi hiyo ya kundi A iliyochezwa Uwanja wa Nyumbu
mkoani Pwani, washindi ambao kwa matokeo hayo wamejiweka katika nafasi
nzuri ya kucheza 16 bora walikuwa mbele kwa mabao 3-0.
Waliotikisa
nyavu ni Anthony Christian dakika ya 23 na 50, Edward Songo dakika ya
27, 75 na 86 na Sunday Leonard dakika ya 32 na 60. Mabao ya Lindi
yalifungwa na Salum Mnyamwile dakika ya 18 kwa njia ya penalti na
lingine dakika ya 48 kupitia kwa Mwarami Maundu.
Nayo
Tanga imepata ushindi wake wa kwanza katika michuano hiyo baada ya
kuifunga Manyara mabao 2-0 katika mechi ya kundi B iliyochezwa Uwanja wa
Tamco mkoani Pwani. Mabao ya washindi yalifungwa na Mbwana Musa dakika
ya 47 na Issa Mwanga dakika ya 60.
Katika
mechi tatu zilizotangulia Tanga ilitoka sare ya mabao 3-3 na Morogoro,
ikapata sare nyingine ya 1-1 dhidi ya Mwanza, na baadaye 1-1 na Tanga.
Kagera
imeendelea kujitutumua katika michuano hiyo baada ya kupata ushindi
wake wa pili katika kundi D kwa kuilaza Kusini Unguja bao 1-0 katika
mchezo uliochezwa Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe jijini Dar es
Salaam.
Bao
lake lilifungwa dakika ya 76 na Novati Sebastian. Mechi iliyopita
Kagera iliifunga Tabora mabao 2-0 baada ya kuteleza katika mechi mbili
za kwanza kwa kufungwa na Kilimanjaro na Singida.
Mechi
nyingine ilichezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambapo
Kinondoni iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mara.
0 comments:
Post a Comment