Mwinyi Hamadi kushoto na Saleh Abdallah |
Na Prince Akbar
ROBO fainali ya michuano ya vijana chini ya umri wa 17,
Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Rollingston inayoshirikisha academy
mbalimbali, zinafanyika leo nchini Burundi.
Katika hatua hiyo, Tanzania imeonyesha kuwa na msingi mzuri
wa soka ya vijana kutokana na kufanikiwa kuingiza timu sita katika hatua ya
Robo Fainali ya michuano hiyo, ambayo awali ilikuwa ikifanyika mjini Arusha.
Timu zilizoingia hatua hiyo ni Azam FC ya Dar es Salaam, JKT
Ruvu ya Pwani, Mjini Magharibi ya Zanzibar, Coastal Union ya Tanga na Bishop
Dunhill na Rollingston za Arusha.
Robo Fainali zote zinachezwa leo Jumanne katika viwanja
viwili tofauti, Aigle Noir ya Burundi
ikimenyana na JKT Ruvu, Ecofoot ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)
ikimenyana na Bishop Dunhill Uwanja wa Gisenyi, wakati Azam FC itamenyana na
Mjini Magharibi, Rollingston na Coastal Union Uwanja wa Nyanza.
Mechi za kwanza zitachezwa saa 7:00 mchana na za pili
zitachezwa saa 9:00 alasiri.
ROBO FAINALI
ROLLINGSTON:
(Julai 17, 2012)
Aigle Noir (Burundi) v JKT Ruvu
Azam FC v Mjini Magharibi
Rollingston v Coastal Union
Ecofoot (DRC) v Bishop Dunhill (Arusha)
0 comments:
Post a Comment