Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya
REAL MADRID WAELEKEA KUCHEMSHA DAU LA LUCA MODRIC
MWENYEKITI wa Real Madrid, Florentino Perez amesema vigogo hao wa Hispania hawatatoa zaidi ya pauni Milioni 27 kumsajili Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26, licha Spurs watamtoa Mcroatia huyo tu kwa dau la pauni Milioni 35.
KLABU ya Spurs inamtaka kiungo wa Hispania, Santi Cazorla, mwenye umri wa miaka 27, kama mbadala wa Modric iwapo akiondoka White Hart Lane.
Tottenham pia imeanza mipango ya kumsajili kipa wa Lyon na Ufaransa, Hugo Lloris, mwenye umri wa miaka 25, atue White Hart Lane, lakini mpango huo unakwazwa na dai la klabbu yake kutaka pauni Milioni 16.
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger atawatuma skauti wake kwenda kumtazama kiungo Mbrazil, Ganso, mwenye umri wa miaka 22, katika mechi ya yao na Uingereza Ijumaa, London ambako inafanyika Michezo ya Olimpiki 2012.
Lakini Wenger ataghairi kumuuza mshambuliaji Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 28, kwa wapinzani wao, Manchester United.
Pamoja na hayo, Arsenal imemuorodhesha mshambuliaji wa Hispania, Fernando Llorente, mwenye umri wa miaka 27, iwapo Van Persie atashindwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.
KLABU ya Chelsea inatazamiwa kumleta Hazard mwingine katika Ligi Kuu ya England, kutokana na mpango wake wa kutaka kumsajili mdogo wake, Eden, aitwaye Thorgan, mwenye umri wa miaka 19, kutoka Lens.
Roberto Di Matteo ameweka wazi Stamford Bridge kuhusu Florent Malouda, mwenye umri wa miaka 32, mmoja wa wachezaji watano ambao wanaweza kuondoka.
ADEBAYOR AWAPIMA SPURS
KLABU ya Tottenham imejaribiwa na washauri wa Emmanuel Adebayor, kuboresha mkataba wao na mshambuliaji huyo wa Manchester City.
DAVID VILLA AREJEA KAZINI...
MSHAMBULIAJI wa Barcelona, David Villa, mwenye umri wa miaka 30, ameanza mazoez baada ya kupona maumivu yake, akimuacha kipa Jose Manuel Pinto kwenye wado ya majeruhi ya Barca.
0 comments:
Post a Comment