Ramadhani Shauri |
Na Prince Akbar
SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa (IBF) limetangaza rasmi
mpambano kati ya bondia Ramadhani Shauri wa Tanzania na Sande Kizito kutoka
Uganda. Mpambano huo utafanyika kutafuta bingwa wa “IBF Continental Afrika”
katika uzito wa Unyoya (Featherweight) kilo 58 katika ukumbi wa Diamond Jubilee
jijini Dar-Es-Salaam.
Bondia Ramadhani Shauri anatoka katika kundi la kocha Mzazi
lenye makao yake makuu Ubungo katika eneo la Mabibo. Shauri ana rekodi ya
mapabano 12 ambapo katika maisha yake ya ngumi ameshinda mara 11na kupoteza
mara 1. Naye bondia Sande Kizito ana rekodi ya mapambano 12 ambapo ameshinda
mapamambano 7 na kupoteza 9.
Aidha, bondia Nasibu Ramadhani atapambana na bondia Twalibu
Mubiru toka Kenya kugombea mkanda wa “IBF East & Central Africa” katika
uzito wa Bantam. Nassibu Ramadhani ana rekodi ya mapambano 9 na kupoteza mara 2
wakati Twalib Mubiru ana rekodi ya mapambano 11 amepoteza mara 7 na kutoka draw
mara 2.
Mpambano kati ya Ramadhani Shauri na Sande Kizito unafanyika
wakati Tanzania ikijijenga katika medani ya michezo ya kimataifa. Tayari Rais
Jakaye Mrisho Kikwete ameshakutana na viongozi wa vyama na taasisi mbalimbali
za michezo kujadili programu za kuiendeleza michezo hapa Tanzania.
Promota wa mpambano huo mkubwa uliopewa jina la “The Rumble
in the City” ni mfanyabiashara maarufu katika jiji la Dar-Es-Salaam Lucas
Rutainurwa wa kampuni maarufu ya Kitwe General Traders ya jijini Dar-Es-Salaam.
Kampuni hii ndiyo iliyopromoti mpambano mwingine wa IBF
mwezi wa Aprili ambapo ulimshughudia bondia machachari wa Tanzania anayejiita
kuwa mbunge wa Rorya kwa wakazi wa jimbo hilo wanaoishi katika jijini
Dar-Es-Salaam Manda Maugo akipoteza katika raundi ya nane!
Nalo Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) lilizindua
program maalum ya “Utalii wa Michezo” katika mkutano wake wa 29 uliofanyika
mwezi wa Juni uliofanyika katika jijini la Honolulu jimbo la Hawaii nchini
Marekani ambayo imelenga kuinua mchezo wa ngumi katika bara la Afrika wakati
nchi za Ghana na Tanzania ni nchi za mfano (Pilot Countries).
Katika programu hii ya “Utalii wa MIchezo” IBF mbali na
kuwapa nafasi mabondia kadhaa toka Tanzania na Ghana kugombea mikanda
mbalimbali itaendesha pia programu ya mikutano yake hapa Tanzania na kuwaleta
wanachama wake kupanda wa mlima Kilimanjaro kila mwaka. Programu hii itawaleta
watalii wengi nchini Tanzania na kutangaza vivutio vya kitalii kupitia michezo.
Tayari bondia Helen Joseph wa Ghana anategemea kupanda
ulingoni Agosti 11 kupambana na bondia Dahianna Santana wa Dominican Republic
kugombea mkanda wa dunia katika uzito wa unyoya (Featherweight) upande wa
wanawake. Mpambano huo utafanyika wiki mbili kabla ya mpambano wa Ramadhani
Shauri ya Sande Kizito.
Wakati huo huo promota wa mpambano huo bwaan Lucas
Rutainurwa akizungumza na mwandishi wa habari hii alisema kuwa ameamua kuwekeza
katika “Utalii wa Michezo” ili kuwawezesha vijana kujiajiri na kujenga uchumi
wa nchi ya Tanzania.
Rutainurwa alisema kuwa ana ratiba ya mapambano ya ubingwa
wa Afrika kila baada ya miezi miwili mwaka huu na mwak akesho ambayo itaipa
Tanzania nafasi ya kunyanyua medani ya michezo pamoja na kuwawezesha vijana
kujiajiri.
Ameziomba kampuni pamoja na watu wenye mapenzi mema
kujitokeza kwa wingi kusaidia kufadhili mapamnano haya ili kuiwezesha Tanzania
kuinuka kimichezo.
0 comments:
Post a Comment