Rais wa Mazembe, Moise Katumbi |
Na Prince Akbar
MAKAMU wa Rais wa Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mohamed Kamwanya amesema kwamba Thomas Emmanuel
Ulimwengu anachelewa kuingizwa kwenye kikosi cha kwanza kwa sababu kiwango
chake bado.
Thomas Ulimwengu |
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwa simu kutoka Lubumbashi jana,
Kamwanya alisema kwamba, Ulimwengu kila anapopewa ruhusa ya kurejea Tanzania
kujiunga na timu za taifa, kwanza huchelewa kurudi Lubumbashi na pia hurudi
akiwa hayuko fiti.
“Hicho ndio kinamchelewesha, lakini kama siyo hivyo angekuwa
anacheza tu kama mwenzake. Na nyinyi watu wa vyombo vya habari mtusaidie, kwa
sababu wachezaji wakija huko wanafanya anasa, wanarudi huku hawako fiti, sasa
inakuwa mbaya,”alisema Kamwanya.
Akiwa anaingia msimu wa pili tangu asajiliwe na Mazembe,
lakini Ulimwengu bado yupo kwenye kikosi cha wachezaji wa akiba wa timu hiyo na
hachezi Ligi Kuu wala Ligi ya Mabingwa, kama mwenzake Mbwana Ally Samatta
ambaye anang’ara.
Akimzungumzia Samatta juu ya habari kwamba kuna klabu zinamataka
Ulaya, Kamwanya alisema kwamba hadi sasa Mazembe haijapokea ofa yoyote kutoka
kwa wakala au klabu na hawawezi kujadili mambo yanayozungumzwa au kuandikwa
kama tetesi.
“Tutakuwa tayari kusema, iwapo tutapata ofa ya maandishi,
lakini kwa sasa tunasema Samatta tupo naye tu ni mchezaji wetu tegemeo,”alisema
Kamwanya.
0 comments:
Post a Comment