Askari wa Polisi wasiojua utaratibu wao wa kazi, usiku wa
leo wamemnyima mwanamuziki Diamond fursa ya kupigwa picha wakati anatumbuiza
kwenye Tamasha la Matumaini, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Pamoja na kwamba waandaaji wa tamasha hilo, walitoa kadi
maalum kwa Waandishi, ili wawe huru kwenye kufanya kwao kazi, lakini ulipowadia
wakati wa Diamond kupanda jukwaani, askari waliwazuia wapiga picha.
Wapiga picha walioruhusiwa ni wa kampuni ya Global Publishers
tu, ambao wameandaa tamasha hilo, lakini BIN ZUBEIRY na mshkaji wa Mwananchi,
walikuwa miongoni mwa walitolewa nishai kinoma noma na marungu juu.
Moja ya vivutio vikubwa katika shoo hiyo pamoja ‘makorokoro
yooootee’ ni Diamond na Chameleon. Wakati Chameleon anatumbuiza, askari
hawakufukuza waandishi na hivyo alipigwa picha kibao, ila alipopenda Diamond
ndipo mizengwe ikaanza na ndiyo maana huwezi kuona picha yake hata moja hapa kutoka shoo ya leo.
Kwa wapenzi wa Diamond wanaotaka kujua kijana huyo alifanya
nini kwenye tamasha hilo, wanunue magazeti ya Global kuanzia Jumatatu na pia
watembelee na tovuti ya kampuni hiyo, kwani wapiga picha wao ndio pekee
waliruhusiwa kupiga picha msanii huyo akitumbuiza. Picha hii ni kutoka Maktaba ya BIN ZUBEIRY
|
0 comments:
Post a Comment