// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PIGO YANGA; NYOTA WATATU WAUMIA, KUTOCHEZA KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PIGO YANGA; NYOTA WATATU WAUMIA, KUTOCHEZA KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, July 16, 2012

    PIGO YANGA; NYOTA WATATU WAUMIA, KUTOCHEZA KESHO


    Kocha wa Yanga, Tom Saintfiet

    Na Prince Akbar
    PIGO Yanga. Wachezaji watatu tegemeo wa klabu hiyo ni majeruhi na hawatacheza mechi ya kesho dhidi ya Waw Salaam ya Sudan Kusini katika klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
    Akina nani hao? Ni kipa Ally Mustafa Barthez, beki Juma Abdul na kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda.
    Nani kasema? Ni kocha Mkuu wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet alipozungumza na BIN ZUBEIRY mchana wa leo juu ya maendeleo ya kambi yake.
    Mtakatifu Tom amesema anasikitika mno alipanga kumuanzisha Barthez katika mechi tya kesho, lakini kwa kuwa ameumia sasa atalazimika kuanza Mghana Yaw Berko tena aliyetunguliwa mawili, Yangva ikilala 2-0 mbele ya Atletico FC ya Burundi juzi.
    Tom amethibitisha watatu hao wote, Barthez, Juma Abdul na Haruna hawatapewa jezi kwenye mechi ya kesho kwa kuwa wanaendelea na tiba na hata leo wameshindwa kabisa mazoezi.
    Sasa Yanga inabakiwa na wachezaji 17 walio fiti, ambao ni kipa; Yaw Berko, mabeki;, David Luhende, Kelvin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Godfrey Taita, Ladislaus Mbogo, Oscar Joshua na Stefano Mwasyika, viungo; Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo, Juma Seif ‘Kijiko’, Shamte Ally, Nizar Khalfan na Idrisa Assenga na washambuliaji; Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Jerry Tegete.
    Yanga inahitaji lazima kushinda mechi ya kesho, ili kufufua matumaini ya kutetea ubingwa wao, baada ya juzi kuanza vibaya kwa kuchapwa 2-0 na Atletico.
    Kikosi cha Yanga, Barthez wa kwanza kulia waliosimama na Juma Abdul ni wa katikati walioinama

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO YANGA; NYOTA WATATU WAUMIA, KUTOCHEZA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top