Salim Kinje |
Na Princess Asia
KIUNGO Salim Kinje ataikosa mechi ya keshokutwa ya Simba
dhidi ya Ports ya Djibouti, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la
Kagame Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutokana na kuwa majeruhi.
Daktari wa Simba SC, Cossmas Kapinga ameiambia BIN
ZUBEIRY mchana wa leo kwamba, Kinje aliumia misuli kwenye mechi na
Azam, Fainali ya Kombe la Urafiki wiki iliyopita na pamoja ya kujilazimisha
kuendelea kucheza, lakini imefikia wakati anahitaji mapumziko.
Kapinga alisema leo Kinje ameshindwa kabisa kufanya mazoezi
ya pamoja na wenzake na ikabidi afanye mazoezi maalum ya peke yake kulingana na
maumivu yake. Kapinga amethibitisha Kinje hatacheza Jumatano na Ports katika
mechi ambayo Wekundu wa Msimbazi, wanatakiwa lazima kushinda ili kufufua matumaini
ya kuingia Robo Fainali ya michuano hiyo, baada ya kuanza vibaya jana kwa
kufungwa 2-0 na URA ya Uganda.
0 comments:
Post a Comment