Mussa Mudde kulia akiwa na jamaa gani sijui... |
KIUNGO wa Simba SC, Mussa Mudde ameumia kifundo cha mguu na jana
baada ya kufanyiwa vipimo katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam, imeelezwa
anatakiwa kuwa nje ya Uwanja kwa wiki mbili.
Daktari wa mmoja wa Muhimbili, ameiambia BIN
ZUBEIRY asubuhi hii kwamba kiungo alifikishwa hospitalini hapo jana saa
1.00 usiku kitengo cha mifupa na kufanyiwa uchunguzi na kubainika ameumia kifundo
cha mguu wa kushoto na itamchukua kiasi cha wiki mbili kupona.
Hii inamaanisha Mudde atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki
zisizopungua tatu, kwani baada ya wiki mbili za kulala tu kitandani, atakuwa na
wiki moja ya kuanza mazoezi ya taratibu.
Huyo anakuwa mchezaji wa pili wa Simba kuumia katika Klabu
Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya awali Amir
Maftah kuumia kidole na kupewa wiki mbili za kuwa nje ya mashindano.
Simba ilitolewa katika Robo Fainali ya Kagame, baada ya kufungwa
mabao 3-1 na Azam FC jana, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kuelekea mwanzo wa msimu mpya wa Ligi Kuu, hakika hili ni
pigo kwa Simba, kwani tayari beki mwingine wa klabu hiyo, Nassor Masoud ‘Chollo’
ni majeruhi wa muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment