Nizar Khalfan |
Na Prince Akbar
KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan aliyesajiliwa
na Yanga msimu huu, ambaye awali ilielezwa atakuwa nje ya Uwanja kwa wiki sita
baada ya kuumia nyonga, amepona kwa ‘Nguvu za Mungu’ na ameorodheshwa kwenye
Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inayotarajiwa
kaunza saa 10:00 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Meneja wa Yanga, Hafidh Suleiman ameiambia BIN
ZUBEIRY mida hii kwamba, Nizar amepona na ataanzia benchi kwenye mechi
ya leo dhidi ya Azam.
Mapema jana, kocha wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet aliiambia
BIN
ZUBEIRY kwamba Nizar alionyesha dalili za kupona mapema awali, lakini
sasa imegundulika anatakiwa kuwa nje ya Uwanja kwa wiki zisizopungua sita.
Kwa masikitiko makubwa, Tom alisema; “Nizar hatacheza
fainali, alionekana kuwa vizuri siku chache zilizopita, sasa atakuwa nje kwa
wiki zisizopungua sita,”alisema.
Tayari Nizar amekosa mechi mbili za Robo Fainali na Nusu
Fainali ya michuano hiyo, licha ya kuanza vizuri katika hatua ya makundi.
Kiungo huyo alisajiliwa na Yanga miezi miwili iliyopita akitokea Philadelphia
Union ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS), ambayo alijiunga nayo kutoka Vancouver
Whitecaps ya Canada, ambayo ilikuwa inacheza MLS.
0 comments:
Post a Comment