KIUNGO
wa Kimataifa raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima Fabregas amerejea jana
usiku na kujiunga na Kikosi cha Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati
Young Africans Sport Club (YANGA) katika mazoezi yanayotarajiwa kuanza
leo jioni saa kumi katika uwanja wa Kaunda Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na tovuti ya klabu www.youngafricans.co.tz kiungo
huyo amesema kuchelewa kwake kulitokana na matatizo binafsi yaliyokuwa
yamemkuta wakati akiwa nchini kwao na kusababisha kuchelewa kujiunga na
Kikosi chake.
Haruna
amewataka wachezaji wenzake kurejesha heshima kwa mara nyingine kwa
kutwaa kombe la Kagame katika michuano inayotarajiwa kuanza Julai 14
Mwaka huu, huku Yanga ikiwa ndiyo Mabingwa watetezi wa michuano hiyo.
Niyonzima
amesema tangu alipokuwa mapunziko alikuwa akifuatilia kwa karibu juu ya
Klabu yake ya Yanga hasa katika zoezi la usajiri unaoendelea na
kupongeza usajili huo kutokana na baadhi ya wachezaji anaowafahamu
kusajiriwa katika kikosi hicho.
Yanga itaanza
kutupa karata yake dhidi ya Atletico ya Burundi ambapo mechi hiyo ndiyo
itakayokuwa ni pekee wakati wa ufunguzi itachezwa katika uwanja wa
Taifa,Jijini Dar es Salaam huku Simba ikaanza kampeni siku inayofuata.
Mabingwa hao watetezi kundi lake limejumuisha na timu za Wau Salaam ya Sudan,Altetico ya Burundi na APR ya Rwanda.
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu wa BARAZA la vyama vya Soka Afrika Mashariki na
Kati (CECAFA), Nicholous Musonye amesema mpaka sasa mdhamini ni mmoja
aliyejitosa kwenye michuano hiyo ambaye ni Rais wa Rwanda,Paul Kagame.
Jumla
ya timu 12 zitashiriki katika michuano hiyo ambayo itaanza Julai 14
hadi Julai 28 ambapo wawakilishi hao watatoka katika nchi za
Tanzania,Uganda,DR Congo,Djibout,Zanzibar,Kenya,Sudan Kusini,Rwanda na
Burundi.(Mwandishi wetu Louis Sendeu)
0 comments:
Post a Comment