Kikosi cha Simba SC |
Na Princess Asia
MICHUANO ya Kombe la Urafiki, imeendelea usiku huu kwa timu
Super Falcon kuilaza Jamhuri ya Pemba bao 1-0 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Super Falcon ilipata bao hilo kupitia kwa Mbarouk Marshed
dakika ya 44, aliyefumua shuti kali na kujaa nyavuni.
Kwa matokeo hayo, Falcon inaongoza Kundi B, kwa pointi zake
tatu, mabao mawili ya kufunga na moja la kufungwa.
Ikumbukwe kundi hilo, limebaki na timu mbili tu, baada ya
kuondolewa kwa Yanga kwenye michuano hiyo kwa kitendo chao kupeleka timu B,
badala ya timu A.
Maana yake, timu zote za kundi hili zimekwishasonga Nusu Fainali
na sasa zinasubiri mechi za kesho za Kundi A, kati ya Azam na Mafunzo na Simba dhidi
ya timu ya taifa ya vijana ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 23, Karume Boys.
Katika mechi za awali za Kundi A, Simba SC ilitoka sare ya
1-1 na Azam FC jana.
Simba ilitangulia kupata bao dakika ya 35 kupitia kwa
mshambuliaji wake iliyemsajili kutoka Dong Tam Long An ya Vietnam, Danny
Mrwanda, lakini Azam ilisawazisha kupitia kwa George Odhiambo ‘Blackberry’
dakika ya 45.
Katika mechi yake ya kwanza juzi, Simba SC ilianza vyema
baada ya kuifunga Mafunzo mabao 2-1, wakati Azam ililazimishwa sare ya 1-1 na
U23, Karume Boys.
Simba sasa inaongoza kundi hilo kwa pointi zake nne, mabao
matatu ya kufunga na mawili ya kufungwa, wakati Azam FC ni ya pili kwa pointi
zake mbili
0 comments:
Post a Comment