Simba; Watacheza na All Stars Jumatatu |
Na Prince Akbar,
MECHI ya Kundi B, Kombe la Urafiki, kati ya Zanzibar All
Stars na Jamhuri imemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bila kufungana jioni hii Uwanja wa Amaan, Zanzibar na kwa
maana hiyo, Simba itacheza na All Stars katika Nusu Fainali Jumatatu, wakati
Azam itacheza na Super Falcon.
Jana usiku, Simba ilimaliza mechi zake za Kundi A ikiwa
kileleni, baada ya bao
pekee la mshambuliaji wake wa kimataifa wa Zambia, Felix
Mumba Sunzu Jr. dakika ya 58 kuwapa ushindi dhidi ya timu ya taifa ya vijana ya
Zanzibar chini ya umri wa miaka 23, Karume Boys.
Katika mchezo wa awali jana, Azam ilifanikiwa kutinga Nusu
Fainali baada ya kuifunga Mafunzo, mabao 3-2.
Mabao ya Azam yalifungwa na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ dakika
ya sita, baada ya kupiga kona iliyotinga moja kwa moja nyavuni, kabla ya Kipre
Tcheche kuunganishia nyavuni krosi ya Abdulhalim Humud ‘Gacuho’ dakika ya 37 na
Ibrahim Mwaipopo kupiga la tatu dakika ya 83.
Mafunzo, ambayo imepangwa kundi moja na Azam katika Kombe la
Kagame, michuano inayotarajiwa kuanza wiki ijayo, mabao yake yalifungwa na
Mohamed Abdulrahman dakika ya 46 na Jaku Joma dakika ya 62.
Smba imemaliza kama kinara wa Kundi A, kwa pointi zake saba,
ikishinda mechi mbili na kutoa sare moja, ikifuatiwa na Azam iliyomaliza na pointi
tano, baada ya kushinda mechi hiyo moja tu na kutoa sare zote dhidi ya U23 ya
Zanzibar, maarufu kama Karume Boys na Simba SC, wakati Mafunzo imeaga bila ya
kuokota hata pointi moja, baada ya kufungwa mechi zote na Azam, Karume Boys na
Simba. Karume imemaliza na pointi nne na imetolewa.
0 comments:
Post a Comment