Na Princess Asia
FAINALI ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 inayozikutanisha
timu za Mwanza na Morogoro itachezwa leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
Dar es Salaam kuanza saa 9 kamili alasiri.
Mwanza ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga
Temeke mabao 3-1 wakati Morogoro iliiondoa Tanga kwenye nusu fainali kwa
ushindi wa mabao 3-1. Mechi zote za nusu fainali zilichezwa Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume juzi.
Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya Temeke na Tanga
itachezwa kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 5 asubuhi. Mashindano ya Copa
Coca-Cola 2012 yalianza Juni 24 mwaka huu yakishirikisha mikoa 28 ya Tanzania
Bara na Zanzibar.
Wakati huo huo: Kozi ya makocha wa mpango wa grassroots
unaolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia
miaka 6-12 inafungwa asubuhi ya leo kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF).
Makocha hao walianza kunolewa Julai 10 mwaka huu kwenye
ukumbi wa Msimbazi Center, Dar es Salaam na wakufunzi kutoka Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wakiongozwa na Gouinden Thandoo.
Washiriki wa kozi hiyo walikuwa 35 ambao ni makocha wa timu
mbalimbali zilizoshiriki mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma wa Shule za
Msingi Tanzania (UMITASHUMTA).
0 comments:
Post a Comment