// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NI MANJI NA SANGA MABOSI WAPYA YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NI MANJI NA SANGA MABOSI WAPYA YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, July 16, 2012

    NI MANJI NA SANGA MABOSI WAPYA YANGA


    Manji kulia akiteta na Sanga kushoto

    Zoezi la uchaguzi wa Yanga, limekamilika na Yussuf Mehboob Manjia meshinda Uenyekiti wa klabu hiyo, wakati Clement Sanga amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na nafasi za Ujumbe Abdallah Bin Kleb, Aaron Nyanda, Mussa Katabaro na George Manyama.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Klabu ya Yanga, Jaji John Mkwawa kushoto akiwa na Mjumbe wa kamati hiyo Mzee Mzimba













    Akitangaza matokeo hayo, majira ya saa 10:30 alfajiri katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga Jaji John Mkwawa amemtangza Manji kama mishindi wa nafasi ya uenyekiti kufuatia kupata asilimia 97% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi hiyo.
    Mwenyekti mpya wa Yanga, Yusuf Manji akiwa na Makamu wake Clement Sanga 
    Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Clement Sanga aliyejipatia asilimia 62% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi ya u makamu mwenyekiti.
    Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na George Manyama  wamechaguliwa katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya  Utendaji.
    Jaji Mkwawa amewashukuru wana Yanga kwa kuwa wastaarabu na watulivu, kitu kilicholekea kufanyika uchaguzi kwa amani na zoezi hilo kumalizika salama pasipo kuwa na rabsha yoyote.
    Matokeo kamili ya wagombea ni:

    Nafasi ya Mwenyekiti:
    Yusuf Manji (kura 1876)  97.0%,  John Jembele (kura 40) 2.6%,  Edgar Chibura (kura 4) 0.24%

    Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
    Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%, Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%

    Nafasi ya Ujumbe: 
    Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro (kura 1068), Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295),  Graticius Ishengoma (kura 247),  Jumanne Mwamenywa (kura 251),  Justine Baruti (610),  Lameck Nyambaya (kura 425),  Omary Ndula (kura 170),  Peter Haule (441),  Ramadhan Said (249),  Yono Kivela (123)

    kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni
    Mwenyekiti: Yusuf Manji,
    Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
    Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI MANJI NA SANGA MABOSI WAPYA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top