Frank Damayo, kiungo wa Ngorongoro |
Na Princess Asia
TIMU ya soka ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka
20, Ngorongoro Heroes leo imefungwa mabao 2-1 na Rwanda Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, ambao ulikuwa wa marudiano ndani
ya siku tatu, baada ya juzi.
Katika mechi hiyo ya kujipima nguvu kwa Ngorongoro Heroes
inayofundishwa na Kocha Jakob Michelsen kabla ya kucheza na Nigeria katika
mechi za mchujo za michuano ya Afrika, mabao ya Nyigu Wadogo yalitiwa kimiani
na Nshimiyimana Emran katika dakika za pili na 30, wakati bao la kufutia
machozi la Rwanda lilifungwa na Atupele Green dakika ya 71.
Ngorongoro Heroes ambayo katika raundi ya kwanza ya michuano
hiyo iliitoa Sudan itacheza mechi ya kwanza ya raundi ya pili Julai 29 mwaka
huu dhidi ya Nigeria kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Rwanda ambayo inaundwa na wachezaji wengi
waliocheza fainali za Kombe la Dunia kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17
miaka mitatu iliyopita tayari, mechi ya kwanza juzi Uwanja wa Chamazi,
iliifunga Ngorongoro 1-0.Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania 'Ngorongoro Heroes', Ramadhan Singano akiwatoka mabeki wa timu ya taifa ya Vijana ya Rwanda katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Picha na Habari Mseto Blog.
Kiungo wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania ‘Ngorongoro Heroes’ Omega Seme (kulia) akichuana na mshambuliaji wa Rwanda, Ruhinda Saifi
Kiungo wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania ‘Ngorongoro Heroes’ Omega Seme (kulia) akichuana na mshambuliaji wa Rwanda, Ruhinda Saifi katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Ngorongoro Heroes inajiandaa na mashindano ya Rwanda ilishinda 2-1.
0 comments:
Post a Comment