Christopher Edward wa Ngorongoro |
Na Princess Asia
TIMU ya soka ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20,
Ngorongoro Heroes leo inashuka dimbani kucheza na Rwanda 'Nyigu Wadogo' Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, ambao ni wa marudiano ndani
ya siku tatu.
Mechi hiyo ya kujipima nguvu kwa Ngorongoro Heroes
inayofundishwa na Kocha Jakob Michelsen kabla ya kucheza na Nigeria katika
mechi za mchujo za michuano ya Afrika itaanza saa 10 kamili jioni.
Ngorongoro Heroes ambayo katika raundi ya kwanza ya michuano
hiyo iliitoa Sudan itacheza mechi ya kwanza ya raundi ya pili Julai 29 mwaka
huu dhidi ya Nigeria kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Rwanda ambayo inaundwa na wachezaji wengi waliocheza fainali
za Kombe la Dunia kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 miaka mitatu
iliyopita tayari, mechi ya kwanza juzi Uwanja wa Chamazi, iliifunga Ngorongoro
1-0.
Viingilio katika
mechi hiyo vitakuwa sh. 2,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani
wakati VIP B na C itakuwa sh. 5,000. Kiingilio kwa VIP A itakuwa sh. 10,000.
0 comments:
Post a Comment