Kikosi cha Ngorongoro cha mwaka juzi |
Na Prince Akbar
TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro
Heroes leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kumenyana na
vijana wenzao wa Nigeria, Flying Eagles katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya
pili kuwania kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri huo,
zitakazofanyika mwakani nchini Algeria.
Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Menmark Jakob Michelsen na Nahodha
wa timu hiyo, kiungo Omega Seme wamesema timu yao iko tayari kwa mechi hiyo
itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Kenya.
Michelsen amesema timu yake imepata mechi mbili za kujipima
nguvu dhidi ya Rwanda, lakini pia aliishuhudia Flying Eagles ikicheza mechi ya
kirafiki na Rwanda (Young Amavubi) uliofanyika Julai 24 mwaka huu jijini
Kigali.
“Timu iko vizuri na
wachezaji kama Frank Domayo, Simon Msuva na Ramadhan Singano ambao pia
wanachezea timu A (Taifa Stars), hivyo uzoefu wao ni muhimu kwa mechi ya kesho.
“Nigeria ni mabingwa watetezi wa michuano hii kwa hiyo
tunatarajia upinzani mkubwa, lakini tumejiandaa kwa hilo. Nigeria ni nchi yenye
mfumo mzuri wa timu za vijana, na sisi tunaelekea huko huko” amesema Michelsen.
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Flying Eagles, John Obuh
amesema haijui vizuri Ngorongoro Heroes lakini anaiheshimu kutokana na ukweli
kuwa inacheza raundi ya pili baada ya kuitoa Sudan katika raundi ya kwanza.
“Sina mchezaji yeyote anayecheza mpira wa kulipwa nje ya
Nigeria, lakini tumekuja kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kucheza
raundi ya mwisho na hatimaye tucheze fainali mwakani,” amesema Obuh
aliyefuatana na nahodha wake Samuel Okan ambaye ni mlinda mlango.
Katika mechi hiyo, itakayochezeshwa na refa Moses Osano, akisaidiwa
na Peter Keireni na Elias Wamalwa, Thomas Onyango mezani, viingilio vitakuwa Sh. 3,000 kwa viti vya
rangi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C itakuwa sh. 5,000. Kiingilio
kwa VIP A ni sh. 10,000.
Osano atasaidiwa na Peter Keireini na
0 comments:
Post a Comment