USO WA MBUZI; Ngassa akiwa kwenye benchi la wachezaji wa akiba Azam kama hahusiki vile |
KOCHA wa Azam FC, Muingereza
Stewart Hall amesema hamtumii Mrisho Khalfan Ngassa kwa sasa, kwa sababu
haonyeshi dalili za kutaka kucheza.
“Hana jitihada zozote,
hajitumi, hana hamu ya kucheza, siwezi kumchezesha,”alisema Stewart mapema tu,
kabla ya mechi ya Robo Fainali dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Pamoja na kucheza bila
Ngassa, Azam imeshinda 3-1 na kuingia Nusu Fainali, ambako itamenyana na AS Vita
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kuna tetesi kwamba,
Ngassa yupo kwenye mgomo baridi kushinikiza uhamisho wa kurejea Yanga, lakini
habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Azam, zinasema kwamba, klabu
hiyo itaendelea kuishi naye hivyo hivyo ‘kimakunyanzi’ hadi amalize mkataba
wake msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment