Kikosi cha Simba kilichocheza na Express jana na kutoka sare ya bila kufungana. Abdallah Juma wa kwanza kushoto waliosimama. |
Na Prince Akbar
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC wameanza vyema michuano ya
Kombe la Urafiki, baada ya kuwafunga wenyeji Mafunzo mabao 2- kwenye Uwanja wa
Amaan, Zanzibar.
Nyota wa mchezo wa leo, alikuwa ni mshambuliaji mpya wa
Wekundu hao wa Msimbazi, Abdallah Juma ambaye alifunga mabao yote hayo.
Abdallah Juma, ambaye amepokewa Simba kama Emmanuel Gabriel
mpya, alifunga bao la kwanza dakika ya 27 akiunganisha pasi muruwa ya Patrick Kanu
Mbivayanga dakika ya 27.
Mshambuliaji huyo mrefu kutoka Ruvu Shooting ya Pwani, alifunga
bao la pili dakika ya 44 kwa kichwa, akiunganisha pasi ya Mbiyavanga tena, kiungo
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Mafunzo walipata bao lao dakika ya 80, mfungaji Jaku Joma.
Katika mchezo wa leo, kwa mara ya kwanza mshambuliaji Danny
Mrwanda aliichezea Simba tangu asajiliwe tena mwezi uliopita akitokea Dong Tam
Long An ya Vietnam.
Simba, mabingwa wa Tanzania walichezesha kikosi chao kamili,
ingawa Emmanuel Okwi, Felix Sunzu na Haruna Moshi ‘Boban’ wameendelea
kukosekana.
Simba; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Amir Maftah/Paul Ngalema,
Lino Masombo, Shomary Kapombe, Amri Kiemba, Danny Mrwanda/Mwinyi Kazimoto,
Mussa Mudde/Paul Ngalema, Abdallah Juma/Uhuru Suleiman, Kanu Mbivayanga/Haroun Othman
na Kiggi Makassy.
Mafunzo: Suleiman Janabi, Hajji Abdi, Ally Juma, Yussuf Makame,
Said Mussa, Juma Othman, Abdulrahim Mohamed, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Ismail
Khamis, Juma Jaku na Ally Othman.
0 comments:
Post a Comment