Na Princess Asia
MWANZA imekata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya
Copa Coca-Cola baada ya leo (Julai 11 mwaka huu) kuitoa Kinondoni kwa penalti
3-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Hadi dakika 90 za mechi hiyo ya robo fainali zinamalizika
timu hizo zilikuwa hazijafunga, hivyo kulazimika kuingia kwenye mikwaju ya
penalti ili kupata mshindi ambaye atacheza nusu fainali keshokutwa (Julai 13
mwaka huu) dhidi ya Temeke.
Walioifungia Mwanza katika penalti ni Christopher Maghinwa,
Steven Lubela na Juma Masunga. Penalti ya Kinondoni ilitiwa wavuni na Shabani
Nyenje. Waliokosa kwa Kinondoni ni Miza Abdallah, John Komba na Juma Masunga.
Nusu fainali ya pili
itakuwa kati ya Morogoro na mshindi wa mechi ya robo fainali kati ya Dodoma na
Tanga itakayochezwa leo jioni (Julai 11 mwaka huu) kwenye uwanja huo huo.
0 comments:
Post a Comment