Mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi akiruka daruga la golikipa wa JKT Ruvu, Shabban Dihile wakati wa mchezo wa kirafiki kwa timu hizo, uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 2-0.
Mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza akimtoka beki wa JKT Ruvu, Paulo Joseph
Beki wa JKT Ruvu, Damas Makwaya akimtoka kiungo wa timu ya Yanga, Haruna Niyonzima wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 2-0.
Mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza akimtoka beki wa JKT Ruvu, Paulo Joseph
Beki wa JKT Ruvu, Damas Makwaya akimnyanyasa mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima (kushoto) akimtoka beki wa JKT Ruvu, Damas Makwaya (katikati) wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 2-0.
Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'canavaro' (kulia) akishangilia kwa staili ya kupeana mikono na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Nizar Khalfan baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza
Na Prince Akbar
KOCHA Mbelgiji Thom Saintfiet leo ameanza kazi vizuri Yanga,
baada ya kuiongoza timu kushinda mabao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wa
kirafiki jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga yalifungwa na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’
dakika ya 18 kwa shuti kali akiunganisha kona ya David Luhend, wakati la pili
lilifungwa na Mwanasoka Bora wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 72,
akiunganisha pasi ya nyota wa Rwanda, Haruna Niyonzima.
Katika mchezo wa leo, ilishuhudiwa mabadiliko ya kiuchezaji
kwenye kikosi cha Yanga, wakicheza soka ya utulivu, bila kukimbia ovyo kama
ilivyo ada yao, muda mwingi wakitulia kwenye eneo lao na kufanya mashambulizi
ya mipango.
Yanga ilitumia mshambuliaji mmoja tu kwenye mchezo wa leo,
Jerry Tegete huku viungo zaidi wakilundikwa uwanjani.
Baada ya mchezo huo, Thom alisema kwamba ameridhishwa na
uchezaji wa timu na matokeo pia na anaamini taratibu timu itazidi kuimarika
hadi kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Alisema baada ya mechi ya leo, atakuwa na vipindi vitatu
zaidi vya mazoezi kabla ya mechi ya ufunguzi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na Kati, Kombe la Kagame Jumamosi dhidi ya Atletico ya Burundi.
Alisema atafanya siku moja moja kuanzia kesho hadi Ijumaa
kabla ya kushusha timu uwanjani Jumamosi kukata utepe wa Kagame. Yanga ndio
mabingwa watetezi wa michuano hiyo, inayoshirikisha timu za Simba na Azam pia
katika orodha ya wenyeji.
Nizar anatia krosi |
Kona langoni kwa JKT |
Kona langoni kwa JKT |
Cannavaro anampongeza Kiiza kupiga la pili |
Mapumziko; Athumani Iddi 'Chuji' anaongoza timu kutoka uwanjani |
Niyonzima akimkumbatia Kiiza kwa kuitumia vema pasi yake |
Shangwe za bao zimeisha vijana wanarudi kazini |
Yaw Berko baada ya kudaka bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa, anakula muziki baada ya mechi |
Mtakatifu Thom anampongeza Nahodha Cannavaro kwa kuwaongoxa vijana vizuri |
Anawapojngeza na marefa pia kwa kuchezesha vizuri |
Hatari langoni kwa JKT |
Mapumziko; Mtakatifu Thom na vijana wake wanaelekea chumbani kubadilishana mawazo kabla ya ngwe ya pili |
Hatari langoni kwa JKT |
Baada ya mapumziko, Niyonzima akimuelekeza Kiiza wakati wanaelekea uwanjani. Kiiza aliingia kipindi cha pili |
Tegete anafumua shuti, lakini Shaabn Dihile alidaka |
Hatari tena langoni kwa JKT |
Said Bahanuzi anachelewa |
0 comments:
Post a Comment