Cheki shughuli yake Sure Boy...Dogo anatisha |
Na Prince Akbar
KIUNGO wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’aliyekuwa
majeruhi amepona na ataichezea timu hiyo katika michuano ya Klabu Bingwa ya
soka Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame, inayoendelea Dar
es Salaam.
Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrisa ameiambia BIN
ZUBEIRY leo kwamba, Sure Boy hivi sasa yuko fiti kwa asilimia 100 na
amerejea kwenye programu ya kocha Muingereza, Stewart Hall.
Mtoto huyo wa winga wa zamani wa kimataifa Tanzania,
Abubakar Salum ‘Sure Boy’, aliumia mwezi uliopita kwenye kambi ya timu ya taifa,
Taifa Stars iliyokuwa inajiandaa na mechi dhidi ya Msumbiji kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani. Stars ilitolewa.
Kuumia kwa Sure lilikuwa pigo si kwa klabu yake tu, bali
hata timu ya taifa, ambako anacheza kwa uelewano mkubwa na kiungo wa Yanga,
Frank Damayo. Vivyo, hivyo kurejea kwake ni faraja kwa Azam na Stars,
inayofundishwa na Mdenmark Kim Poulsen.
Azam iliyoanza kwa sare ya 1-1 na Mafunzo Jumapili, itarejea
uwanjani Julai 21, kumenyana na Tusker FC ya Kenya na tunatarajia ‘mavituuz’
adimu kutoka kwa ‘maji yaliyofuata mkondo’.
0 comments:
Post a Comment