Danny Mrwanda |
Na Princess Asia
MSHAMBULIJI wa Simba SC, Danny Mrwanda amewapoza mashabiki
wa timu hiyo, baada ya kipigo cha jana cha mabao 2-0, kutoka kwa URA ya Uganda
katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame akisema kwamba
safari bado ndefu na mashabiki wasife moyo.
Mrwanda ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba kwa hali na mali,
lengo lake ni kuisaidia timu ishinde, lakini anasikitika hali ya hewa
ilimsumbua sana jana hata akashindwa kutimiza lengo hilo.
“Kwa hali na mali, lengo langu ni kuisaidia timu ishinde,
kwangu hali ya hewa ilikuwa kikwazo, safari bado ni ndefu, msife moyo wana
Simba, mazuri yaja,”alisema Mrwanda
Uhuru Suleiman |
Kwa upande wake, kiungo wa Simba SC, Uhuru Suleiman amesema
kwamba hakupata usingizi usiku wa jana kutokana na kuumizwa kipigo hicho.
“Kiukweli usiku wote wa jana kila nikigeuza ubavu, naiona
game tuliyofungwa jana, hivyo naamini mpo mlioumia kama mimi, hivyo niwatake
radhi mashabiki wote kwa kupoteza mchezo ule, naamini tutafanya vizuri katika
michezo ilyobakia, ahsanteni kwa umoja wenu,”alisema Uhuru.
Simba ilianza vibaya jana Klabu Bingwa Afrika Mashariki na
Kati, Kombe la Kagame, baada ya mabao mawili ya Feni Ally dakika ya 11 na 90+2
kuwanyamazisha 2-0.
Katika mchezo huo, Simba ilicheza vizuri, lakini tu
walishindwa kutumia vizuri nafasi walizopata na mabao yote walifungwa wakitoka
wao kushambulia.
Simba watacheza tena keshokutwa dhidi ya Ports ya Djibouti
iliyofungwa 7-0 na Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika
mchezo wa kwanza, mechi ambayo itatanguliwa na mchezo kati ya Vita Club na URA
ya Uganda.
0 comments:
Post a Comment