Tetesi za J'tano magazeti ya Ulaya
MAN UNTIED YAKWAMA KWA MOURA
KLABU ya Manchester United imefeli jaribio la kumnasa kiungo wa Sao Paulo ya Brazil, Lucas Moura, mwenye umri wa miaka 19, kwa dau la pauni Milioni 29.8, kwa mujibu wa klabu hiyo ya Brazil.
KIUNGO Oscar, mwenye umri wa miaka 20, amewasili London na kikosi cha Brazil cha Olimpiki na atafanyiwa vipimo vya afya kuelekea kusajiliw akwa dau la pauni Milioni 25, akitokea klabu ya Internacional kwenda Chelsea.
MSHAMBULIAJI Dimitar Berbatov anaweza kujiunga na AC Milan au Juventus, kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo wa Manchester United.
KOCHA mpya wa Watford, Gianfranco Zola anamtaka gwiji wa Italia, Filippo Inzaghi, mwenye umri wa miaka 38, na Alessandro Del Piero, mwenye miaka 37, ambao wote kwa sasa ni wachezaji huru.
KLABU ya Barcelona inaweza kumfuata beki wa Liverpool, Daniel Agger baada ya kumkosa kiungo wa Athletic Bilbao, Javi Martinez, mwenye umri wa miaka 23.
MSHAMBULIAJI wa Ufaransa, Bafetimbi Gomis, mwenye umri wa miaka 26, ataachana na mpango wa kuhamia wa Tottenham, ili abaki Lyon.
MSHAMBULIAJI Robin van Persie anajiandaa kwa mazungumzo na kocha wa Arsenal, Arsene Wenger katika msistizo wa kuondoka The Gunners. Mshambuliaji huyo wa Uholanzi, mwenye umri wa miaka 28, ameonyesha nia ya kujiunga na Juventus au Manchester United.
KLABU ya Fulham imeanza mazungumzo ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku, mwenye umri wa miaka 19.
BEKI wa Manchester City, Kolo Toure anaweza kujiuza mwenyewe kwa klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia, ambako atakuwa akipata mshahara wa pauni 50,000 kwa wiki, hiyo ikiwa nje ya kodi na nyumba ya kuishi pamoja na gari mbili atakazopewa, kulipiwa tiketi za ndege na huduma nyingine.
KOCHA wa Sunderland, Martin O'Neill anataka kurejea klabu yake ya zamani, Aston Villa kumsajili James Collins. Villa inajiandaa kumuuza nyota huyo wa Wales mwenye umri wa miaka 28, huku wakiwa karibu kumnasa Mholanzi wa Feyenoord,l Ron Vlaar, mwenye umri wa miaka 27.
KLABU za Everton na West Brom inataka kumsajili beki wa FC Copenhage, raia wa Costa Rica, Bryan Oviedo, mwenye umri wa miaka 22, ambaye amekuwa akifuatiliwa na Manchester United pia.
BEKI Scott Dann anaweza kujiunga na Ajax kwa mkopo kufuatia kushuka daraja kwa Blackburn. Reading na Southampton zimefeli kumsajili beki huyo anayeuzwa pauni Milioni 6.
KIUNGO wa Tottenham, Danny Rose, mwenye umri wa miaka 22, amekubali kuondoka kwa Luka Modric White Hart Lane na amesema sasa hajui mustakabali wake katika klabu hiyo chini ya kocha mpya, Andre Villas-Boas.
KLABU ya Chelsea ipo karibu kumsajili mdogo wake, Eden Hazard,r Thorgan, mwenye umri wa miaka 19, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Michezo wa Lens, Antoine Sibierski.
SUAREZ AWAPIGA VIJEMBE MAN UNITED
MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Luis Suarez, ambaye alifungiwa mechi nane kwa kashfa ya ubaguzi dhidi ya Patrice Evra, amefufua malumbano na beki huyo Mfaransa wa Manchester United, akitumia Televisheni ya Uruguay kusema: "Kwa England, Man United wana nguvu ya kisiasa, na unatakiwa kuheshimu hilo na kufunga mdomo wao."
MSHAMBULIAJI Peter Odemwingie anaweza kuondoka West Brom baada ya kutofautiana na kocha mpya Steve Clarke mazoezini.
KLABU ya Arsenal bado haijaanza mazungumzo ya kujadili mkataba mpya na Theo Walcott, licha ya kuwapo tetesin kwamba winga huyo wa England ataondoka bure msimu ujao.
BEKI mkongwe, David Weir, mwenye umri wa miaka 42, yuko tayari kucheza tena Everton iki3wa atahitajika.
YAYA MPANDA BAISKELI...
MWANASOK bora Afrika, Yaya Toure anafanya mazoezi ya kutumia baiskeli katika klabu yake, Manchester City kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu wakiwa ziarani Austria.
0 comments:
Post a Comment