Moro wakishangilia ubingwa wao pamoja na mfano wa hundi waliyokabidhiwa |
Na Princess Asia
MOROGORO imetwaa ubingwa wa mashindano ya vijana chini ya
umri wa miaka 17, Copa Coca Cola baada ya kuifunga Mwanza bao 1-0, kwenye
Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Shukrani kwake, Salum Ramadhani aliyefunga bao hilo, pekee
dakika ya 36, akiunganisha pasi nzuri ya Mtalemwa Katunzi.
Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Temeke
ilijinyakulia Medali ya Shaba ya michuano hiyo, baada ya kuwafunga Tanga mabao
2-0, yote yakitiwa kimiani na
Rehani Kibingu katika dakika za 48 na 86.
Kwa kutwaa ubingwa, Morogoro wamezawadiwa Sh Milioni 8 na
wadhamini wa michuano hiyo, Coca Cola, wakati Mwanza wamepata Sh. Milioni 4.4
na washindi wa tatu, Temeke wamepata Milioni 3.2.
Katika tuzo binafsi, Kocha wa Tanga, Mohamed Kampira aliibuka
kocha bora, mwamuzi bora alikuwa Liston Hiyari wakati kipa bora alikuwa Shukuru
Mohamed wa Temeke, mfungaji bora Mtelamwa Katunzi wa Morogoro, mchezaji bora ni
Shiza Kichuya, ambapo kila mmoja alipata sh 750,000 huku Tanga ikiondoka na Sh Milioni
1 kwa kuwa timu yenye nidhamu.
Mwanza ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga
Temeke mabao 3-1 wakati Morogoro iliiondoa Tanga kwenye nusu fainali kwa
ushindi wa mabao 3-1. Mechi zote za nusu fainali zilichezwa Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume juzi.
Mashindano ya Copa Coca-Cola 2012 yalianza Juni 24 mwaka huu
yakishirikisha mikoa 28 ya Tanzania Bara na Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment