Na Princess Asia
MJINI Magharibi imetinga hatua ya 16 bora ya michuano ya
Copa Coca-Cola baada ya leo (Julai 4 mwaka huu) kuilaza Tanga bao 1-0 katika
mchezo uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Bao la washindi katika mechi hiyo ya kundi B lilifungwa
dakika ya 68 na Juma Ally. Kwa matokeo hayo Mjini Magharibi ambayo imemaliza
mechi zake imefikisha pointi 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine
katika kundi hilo.
Mbeya imejipatia ushindi wa pili mfululizo katika kundi lake
la C baada ya leo kuifunga Mara bao 1-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa
Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam. Mshambuliaji John Jerome
alifunga bao hilo pekee dakika ya 43.
Licha ya ushindi huo Mbeya wameshindwa kukata tiketi ya 16
bora kwani wamemaliza mechi zao wakiwa na pointi sita tu. Timu za Dodoma yenye
pointi 12 na Kinondoni ambayo imefikisha pointi 10 na mechi moja mkononi ndizo
zilizofuzu kucheza 16 bora kutoka kundi hilo.
Pwani imepata ushindi wake wa kwanza katika kundi lake la D
baada ya leo kuichapa Kagera mabao 3-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa
Nyumbu mkoani Pwani. Mabao ya washindi yalifungwa na Cotiveno Ngaga dakika ya
19, Abdallah Juma dakika ya 30 na Salum Ame dakika ya 68.
Kagera ambayo imebakiza mechi moja dhidi ya Shinyanga ikiwa
na pointi sita ilipata bao dakika ya 42 kupitia kwa Athuman Kassim. Nazo Ruvuma
na Arusha zimetoka suluhu katika mechi ya kundi A iliyochezwa Uwanja wa Tamco.
0 comments:
Post a Comment