Wachezaji wa Simba muda si mrefu wataanza kung'aa na uzi mpya wa maana pigo za Man City |
Na Princess Asia
KLABU ya soka ya Simba jana imepokea msaada wa jezi, raba,
viatu vya kuchezea mpira, mabegi na suti za michezo (tracksuit) – vyote vya
kisasa kabisa, kutoka kwa familia ya Al Ruwahi. Msaada huo umetolewa kwa
mapenzi mema ambayo familia hiyo inayo kwa klabu.
Amesema takribani miaka 30
iliyopita, familia hiihii ilitoa zawadi ya basi (Nissan Coaster) kwa Simba na
kuifanya klabu yetu kuwa ya kwanza nchini kumiliki basi lake yenyewe.
Amesema klabu ya soka ya Simba inatumia nafasi hii kuwakaribisha
wapenzi na wanachama wake kujitokeza kuisaidia klabu kwa namna yoyote ile, kama
ilivyofanya familia hii ya Al Ruwahi, ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya klabu.
"Simba ni ya kila mmoja na haina mwenyewe. Umoja na
mshikamano baina ya viongozi, wadhamini, wapenzi na wanachama wake, ndiyo
utakaoifanya izidi kuwa bora hapa nchini na nje ya mipaka ya taifa letu,"alisema Kamwaga maarufu kama Mr. Liverpool.
Amesema kwa mujibu wa kanuni za mashindano haya, wachezaji wote waliokuwa na kadi moja
ya njano kwenye hatua ya makundi wamefutiwa kadi zao na hivyo Simba itaingia
uwanjani kesho Jumanne kwenye pambano dhidi ya Azam ikiwa haina mchezaji mwenye
adhabu.
Simba imesifiwa na CECAFA kuwa ni miongoni mwa timu zenye
nidhamu nzuri kwenye michuano ya Kagame mwaka huu, mfano ukitolewa kwenye
pambano lake dhidi ya AS VITA ya DR Congo, ambapo hakukuwapo na kadi yoyote
iliyotolewa mechi nzima.
0 comments:
Post a Comment