Michelsen |
Na Prince Akbar
KOCHA wa timu za taifa za vijana za Tanzania, Mdenmark Jakob
Michelsen ameita wachezaji 22 kwa ajili ya michuano ya kimataifa ya Coca-Cola
itakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Baadaye watachujwa na kubaki 16 ambao ndiyo watakaokwenda
kwenye michuano ya Afrika Kusini. Wachezaji waliochaguliwa wametokana na
michuano ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Dar es Salaam na mkoani Pwani
kuanzia Juni 24- Julai 2 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni Abdulrahman Mandawanga (Dodoma),
Abraham Mohamed (Mjini Magharibi), Ayoub Alfan (Dodoma), Bakari Masoud (Tanga),
Daniel Justin (Dodoma), Denis Dionis (Ilala), Edward Songo (Ruvuma), Fikiri
Bakari (Tanga), Hassan Kabunda (Temeke), Joseph Chidyalo (Dodoma), Mutalemwa
Katunzi (Morogoro) na Mwarami Maundu (Lindi).
Wengine ni Nankoveka Mohamed (Ilala), Nelson Peter
(Morogoro), Omari Saleh (Singida), Rajab Rajab (Mwanza), Said Said (Kagera),
Shiza Kichuya (Morogoro), Shukuru Msuvi (Temeke), Tanganyika Suleiman (Kigoma),
Tumaini Baraka (Kilimanjaro) na William John (Ruvuma).
Pia Michelsen ameongeza wachezaji saba kwenye kikosi cha
Serengeti Boys ambacho Septemba mwaka huu kitacheza na Kenya kuwania tiketi ya
fainali za vijana wenye umri chini ya miaka 17 za Afrika zitakazofanyika
mwakani nchini Morocco.
Wachezaji walioongezwa kwenye kikosi hicho ambao pia
wametoka kwenye Copa Coca-Cola ni Abdallah Baker (Mjini Magharibi), Abdallah
Kheri (Mjini Magharibi), Calvin Manyika (Rukwa), Dickson Ambunda (Mwanza),
Hassan Mganga (Morogoro), Miza Abdallah (Kinondoni) na Mzamiru Said (Morogoro).
0 comments:
Post a Comment