Marefa wa Kagame mwaka jana, wakisindikizwa na Polisi kwa usalama wao, baada ya maamuzi yao kutowafurahisha mashabiki |
Na Prince Akbar
BARAZA la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA) limeteua waamuzi 15 kuchezesha michuano ya Kombe la Kagame
itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14-28 mwaka huu.
Waamuzi hao wanatakiwa kuwasili Dar es Salaam, Julai 11
mwaka huu kwa ajili ya vipimo vya afya na mtihani wa utimamu wa viungo
utakaofanyika Julai 12 na 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya
wakufunzi wa CECAFA.
Kwa upande wa waamuzi wa kati (centre referees) walioteuliwa
ni Anthony Ogwayo (Kenya), Dennis Batte (Uganda), Israel Mujuni (Tanzania
Bara), Issa Kagabo (Rwanda), Thierry Nkurunziza (Burundi), Farah Aden Ali
(Djibouti) na Waziri Sheha (Zanzibar).
Waamuzi wasaidizi (assistant referees) ni Elias Kuloba
(Kenya), Peter Sabatia (Kenya), Musa Balikoowa (Uganda), Hamis Changwalu
(Tanzania Bara), Jesse Erasmo (Tanzania Bara), Simba Honore (Rwanda), Abdulahi
Mahamoud (Djibouti) na Josephat Bulali (Zanzibar).
Yanga ndio bingwa wa michuano hiyo, baada ya kuifunga Simba katika fainali 1-0, mwaka jana,
0 comments:
Post a Comment