Manji kushoto akiwa na sanga kulia |
Na Mahmoud Zubeiry
UCHAGUZI Mdogo wa klabu ya Yanga, unafanyika leo kuanzia saa
5:00 asubuhi katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam huku kambi ya
Yussuf Mehboob Manji ikipewa nafasi kubwa ya kushinda.
Manji anayewania Uenyekiti dhidi ya Edgar Chibura na John
Jambele, juzi alitambulisha watu watano anaotaka kuchaguliwa nao leo wakati
alipokuwa akihutubia mamia ya wanachama kwenye Mkutano wa kampeni, Uwanja wa
Kaunda, uliopo makao makuu ya klabu, makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani.
Manji aliwataja watu hao kuwa ni nafasi ya Makamu
Mwenyekiti, Clement Sanga na Wajumbe wanne ni Abdallah Bin Kleb, Mussa
Katabaro, Lameck Nyambaya na George Manyama.
Ikumbukwe uchaguzi huo mdogo unafuatia Wajumbe wengi wa
Kamati ya Utendaji iliyochaguliwa miaka miwili iliyopita, akiwemo Mwenyekiti
Wakili Lloyd Baharagu Nchunga na Makamu wake, Davis Mosha kujiuzulu na
watakaochaguliwa Jumapili watadumu kwa miaka miwili, kumalizia kipindi cha
uongozi cha waliojiuzulu.
Manji aliwaomba wanachama wa Yanga pamoja na kumchagua yeye
Jumapili, pia wawachague na watu hao watano, Sanga, Katabaro, Bin Kleb,
Nyambaya na Manyama, kwani ni watu ambao anaamini atafanya nao kazi vizuri na
kwa ufanisi.
Alisema iwapo akichaguliwa watu hao na mambo yakawa mabaya
klabuni, atakuwa tayari kujiuzulu lakini akasema atasikitika iwapo atachaguliwa
pamoja na watu tofauti nao hao.
Alisema katika kipindi hiki ambacho klabu haina uongozi,
watu hao watano wamekuwa wakimsaidia kujenga timu kama kusajili na kadhalika
kwa kujitolea hivyo ana imani nao kwa kiasi kikubwa.
Shughuli hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa wanachama Vijana
wa Yanga, Bakili Mohamed Makele na Mwenyekiti wa Wazee, Mzee Ibrahim Ally
Akilimali, ambao waliwaomba wana Yanga kuchagua timu hiyo na mambo yatakuwa
mazuri.
Umati wa wanachama wanaokadiriwa kufika 2000 au zaidi
ulihudhuria mkutano huo na wakati wote walikuwa wakishangilia hotuba, kuonyesha
kwamba wanaafiki.
Manji akiwa amemuinua mkono Bin Kleb, wengine kulia ni Manyama na Nyambaya, wakati kushoto ni Sanga |
Manji anahutubia |
Mussa Katabaro anamwaga sera |
Bin Kleb anamwaga sera, alisema yeye si mtu wa maneno, ni mtu wa vitendo |
Nyambaya anamwaga sera |
Manji anamwaga sera |
0 comments:
Post a Comment