|
Manji anaondoka TFF, umati ukimsindikiza |
|
Sura za huzuni; wanachama wakisikitika nje ya ofisi za TFF |
|
Wanachama wakisikitikia pingamizi la Manji |
|
Ni huzuni tupu |
|
Hakuna anayufurahia |
|
Kila mtu ana hasira |
|
Yaani watu wamekasirika ile mbaya |
|
Hadi akina mama wana hasira pia |
|
Manji anatoka chumba cha mahojiano |
|
Anaziacha ofisi za TFF |
|
Anapotea |
|
Anawasalimu wazee |
|
Anajadiliana na wazee |
|
Umati unamsindikiza |
|
Anafunguliwa mlango wa gari lake |
|
Anaingia na kupotea |
Na Prince Akbar
MAMIA ya wanachama wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, leo
wameandamana hadi makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala,
Jijini kupinga pingamizi alilowekewa mgombea Uenyekiti wa klabu hiyo katika
uchaguzi wa Julai 15, mwaka huu, Yussuf Manji.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF, chini ya Mwenyekiti wake, Deo
Lyatto leo ilikuwa inapitia pingamizi mbili walizowekewa wagombea, Manji na Stanley
Kavela ‘Yono’ anayewania Umakamu Mwenyekiti.
Tangu saa nne asubuhi hadi saa nane mchana, Kamati hiyo
ilikuwa inamuhoji Manji ambaye hata alipotoka, ilielezwa alitakiwa kurejea
tena.
Manji alitoka mara mbili na kurejea kufuata vielelezo
alivyotakiwa kuwasilisha kuhusiana na pingamizi alilowekewa, ambalo vyanzo vinasema
ni zito.
Tangu asubuhi wanachama walikuwa ‘kibao’ nje ya Ofisi za
TFF, zilizopo ndani ya Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam wakionyesha
hasira zao dhidi ya pingamizi hilo, ambalo aliloliweka anafanywa siri.
Wanachama walisikika wakisema kwamba kama Kamati ya Lyatto
itamuengua Manji basi hakuna haja ya uchaguzi.
Miongoni mwa waliokuwapo katika wanachama ni wazee wa klabu
hiyo, akina Ibrahim Akilimali, Dk Idrisa Katundu na wengineo, wakiwemo
wanachama maarufu.
Kuna kila dalili kwamba uamuzi wa kumuengua Manji katika
uchaguzi huo litakuwa jambo la hatari kwa klabu hiyo, kwani wanachama tayari
wamekwishajenga imani kubwa juu yake.
Manji mwenyewe alipotoka kwenye chumba cha mahojiano
alionekana asiye na furaha hali ambayo ilizidi kuwatia wasiwasi wanachama
kwamba huenda kikao hakikuwa kizuri kwake.
0 comments:
Post a Comment