// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MANJI ALIKUTANA NA WACHEZAJI KABLA YA KUUA 7-1 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MANJI ALIKUTANA NA WACHEZAJI KABLA YA KUUA 7-1 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, July 17, 2012

    MANJI ALIKUTANA NA WACHEZAJI KABLA YA KUUA 7-1

    Manji akizungumza na wachezaji
    UONGOZI mpya wa klabu ya Yanga leo asubuhi ulitembelea makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na kukutana na kuzungumza na wachezaji. 
    Viongozi hao wapya waliokuwepo kwenye msafara huo ni mwenyekiti, Yussuf Manji, makamu mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wa kamati ya utendaji, Abdalla Bin Kleb, Mussa Katabalo na George Manyama.
    Katika msafara huo, pia walikuwemo wajumbe wa kamati ya utendaji katika uongozi uliopita, Salum Rupia na Mohamed Bhinda.
    Katika kikao chake hicho na wachezaji, Manji aliwataka wawe na imani kubwa kwa uongozi mpya kwa vile wamejipanga vyema kuhakikisha timu inapata huduma zote muhimu na kwa wakati na pia inapata ushindi katika kila mechi watakazocheza.
    Manji aliwaeleza wachezaji hao kuwa, wanapaswa kucheza kwa ari na kujituma kwa vile matatizo yaliyojitokeza msimu uliopita hayatakuwa na nafasi katika uongozi wake.
    Katika kikao hicho, wachezaji wa Yanga walionekana kuwa na furaha kubwa huku kila wakati wakipiga makofi ya kumshangilia mfadhili huyo wa zamani wa klabu hiyo.
    Mbali na Manji, viongozi wengine waliopata nafasi ya kuzungumza na wachezaji ni Sanga na Katabalo, ambao waliwaelezea mikakati mbalimbali ya uongozi wao.
    Manji alichaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Yanga mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuwabwaga Edgar Chibula na John Jambele. Uchaguzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Diamond, Jubilee, Dar es Salaam.
    Uchaguzi huo mdogo uliitishwa baada ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Lloyd Nchunga, makamu wake, Davis Mosha na wajumbe wanne wa kamati ya utendaji huku mmoja akifariki dunia.

    Manji na viongozi


    Wachezaji wakimsikiliza Manji

    Manji akizungumza na wachezaji

    Manji anasalimiana na Chuji, Bin Kleb anafuatia na viongozi wengine

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANJI ALIKUTANA NA WACHEZAJI KABLA YA KUUA 7-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top