Tetesi za J'nne magazeti ya Ulaya
MANCINI AKUBALI YAISHE KWA VAN PERSIE, AWALAUMU MABOSI WAKE
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini ana wasiwasi amepoteza mipango katika mbio za kumnasa mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 28.
NA Mancini amekasirishwa na mabosi wa City kwa kutompa ushirikiano wa kutosha katika mpango wa kumsajili Van Persie.
VIGOGO wa Serie A, AC Milan wameanza mazungumzo na mshambuliaji wa Arsenal, Nicklas Bendtner katika mpango wao wa kumuhamishia Mdenmark huyo Italia.
KLABU ya Manchester United ya England inamuwania kiungo wa River Plate ya Argentina, Ezequiel Cirigliano, mwenye umri wa miaka 20, ambaye anatakiwa pia na klabu za Manchester City ya England na Paris Saint-Germain ya Ufaransa.
MSHAMBULIAJI anayeondoka Manchester United, Dimitar Berbatov, mwenye umri wa miaka 31, anaweza kutimkia Urusi, baada ya Zenit St Petersburg kuonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo.
KLABU ya Bayern Munich inajiandaa kumsajili kiungo wa Manchester City, Nigel de Jong, mwenye umri wa miaka 27, baada ya mpango wa klabu hiyo ya Ujerumani kumsajili mwanasoka wa kimataifa wa Hispania, Javi Martinez kama kuzimika hivi.
KLABU ya Tottenham imejiunga kwenye mbio za kumsajili mchezaji wa zamani wa Liverpool, ambaye kwa sasa anachezea Hoffenheim, Ryan Babel, mwenye umri wa miaka 25, ambaye anawaniwa pia na Swansea na Newcastle.
KLABU ya Fulham anayo pia inaripotiwa kuwa na mpango wa kumsajili Mholanzi, Babel.
KLABU ya Liverpool inajiandaa kukata dau la pauni Milioni 10 kumsajili mshambuliaji wa Swansea, Joe Allen, mwenye umri wa miaka 22.
KLABU ya Zenit St Petersburg imejiunga kwenye mbio za kumsajili beki wa Liverpool, Martin Skrtel, mwenye umri wa miaka 27, na Manchester City na Napoli pia zinamtaka.
KLABU ya Nottingham Forest inataka kumsajili Jermaine Jenas, mwenye umri wa miaka 29, arejee City Ground ambao wanataka kumchukua kiungo huyo Tottenham.
PARKER KISU TENA
NYOTA Scott Parker anatarajiwa kuikosa mechi ya kirafiki ya England na Italia mwezi ujao kutokana na kiungo huyo wa Tottenham kujiandaa kufanyiwa upasuaji ambao akose mechi kadhaa za mwanzoni za Ligi Kuu
0 comments:
Post a Comment