Roberto Mancini sasa mali ya Manchester City 2017
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amesaini mkataba wa miaka mitano kuendelea kuinoa klabu hiyo bingwa Ligi Kuu Englamd.
Mancini alichukua nafasi ya Mark Hughes kama kocha wa City, Desemba mwaka 2009, na kuiongoza timu kutwaa Kombe la FA mwaka 2011.
Mwaka mmoja baadaye, City ilitwaa taji lake la kwanza la Ligti Kuu tangu 1968.
"Manchester City ni klabu nzuri," alisema Mancini katika tovuti ya klabu hiyo. "Niaangalia sana mbele katika changamoto na mambo ya kuvutia mbele yangu."
Mancini alitwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Etihad katika siku ya mwisho wa ligi kimaajabu, kwa mabao ya dakika za majeruhi ya Sergio Aguero yakiiwezesha timu hiyo kushinda 3-2 dhidi ya QPR na kuwapiku wapinzani wao,Manchester United kwa wastani wa mabao.
City wataanza kutetea ubingwa wao nyumbani kwa kumenyana na Southampton Agosti 19, mwaka huu, lakini Mancini pia ana nafasi nyingine ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kampeni yake ya kwanza kwenye michuano hiyo, iliishia kwa kushindwa kufuzu kutoka hatua ya makundi msimu uliopita.
IMETAFSIRIWA KUTOKA BBC SPORT
0 comments:
Post a Comment