// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAN UNITED YATAJA KIKOSI KINACHOKUJA AFRIKA, CHAONDOKA LEO MANCHESTER - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAN UNITED YATAJA KIKOSI KINACHOKUJA AFRIKA, CHAONDOKA LEO MANCHESTER - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, July 16, 2012

    MAN UNITED YATAJA KIKOSI KINACHOKUJA AFRIKA, CHAONDOKA LEO MANCHESTER


    Rio Ferdinand
    15/07/2012 21:26, Report by Gemma Thompson

    KIKOSI cha Manchester United kinachoundwa na mseto wa wachezaji vijana na wakongwe kinaondoka leo kwenda Afrika Kusini kwa ziara ya kujiandaa msimu mpya.
    Kwa mujibu wa tovuti ya klabu hiyo, kikosi hicho cha wachezaji 22 kitaondoka Uwanja wa Ndege wa Manchester kuelekea Durban, ambako United itafungua dimba la ziara yake kabla ya kwenda Cape Town na baadaye China, katika Jiji la Shanghai. Wachezaji wakongwe wakiongoza na Rio Ferdinand - ambaye atakuwa Nahodha wa kikosi katika safari hiyo, Michael Carrick na Paul Scholes wamo kwenye safari wote sambamba na chipukizi kibao, wakiwemo Davide Petrucci, Jesse Lingard na Ryan Tunnicliffe. Mshambuliaji wa Wekundu hao, Bebe pia amejumuishwa kwenye kikosi hicho, baada ya kurejea Old Trafford akitoka kucheza kwa mkopo Besiktas ya Uturuki msimu uliopita.
    Kikosi cha Sir Alex Ferguson kitamenyana na AmaZulu FC mjini Durban Jumatano usiku, kabla ya kumenyana na Ajax Cape Town Jumamosi katika mechi za kirafiki. Wekundu hao katika ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya wataenda pia Norway, Sweden na Ujerumani mwezi ujao - watakwenda Shanghai kumenyana na Shanghai Shenhua Jumatano wiki ijayo. Mechi zote za ziara hiyo zitaonyeshwa na Televisheni ya MUTV na mtandao wa klabu hiyo, MUTV Online.
    KIKOSI CHA ZIARA: Lindegaard, Amos, Johnstone, Ferdinand, Veseli, Vermijl, Wootton, Blackett; Valencia, Anderson, Carrick, Scholes, Powell, Kagawa, Bebe, Tunnicliffe, Lingard, Brady, Petrucci; Berbatov, Chicharito, Macheda.

    MRATIBA ZIARA YA DHL
    J'tano Julai 18  v AmaZulu FC
    J'mosi Julai 21 v Ajax Cape Town
    J'tano Julai 25 v Shanghai Shenhua
    Mechi tatu zaidi zitachezwa Oslo, Gothenburg na Hanover

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YATAJA KIKOSI KINACHOKUJA AFRIKA, CHAONDOKA LEO MANCHESTER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top