Tetesi za J'nne magazeti ya Ulaya
WENGER AONYESHA NIA KWA PAULINHO
KOCH Arsene Wenger amesema Arsenal bado ina dhamira ya kutoa dau la pauni Milioni 9 kumsajili kiungo mpachika mabao, Paulinho, mwenye umri wa miaka 23, kutoka Corinthians ya Brazil.
KLABU ya West Ham inamtaka mshambuliaji wa Manchester United striker Dimitar Berbatov, mwenye umri wa miaka 31, ambaye yuko katika wakati mgumu Old Trafford, baada ya kupoteza namba kwenye kikosi cha kwanza.
MPANGO wa Manchester United kumsajili Lucas Moura umekutana na kikwazo kingine, wakati Sao Paulo ilipoongeza dau la kumuuza mchezaji huyo hadi pauni Milioni 34.
MABINGWA wa Hispania, Real Madrid wanaamini wao ndio klabu pekee, ambayo kiungo wa Tottenham, Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26, anataka kujiunga nayo, na rais, Florentino Pérez, hamewaambia rafiki zake anajiamini kwa kiasi kikubwa kwamba atampata nyota huyo.
MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 23, amewaambia wawakilishi wake kupiga dili la kumrejesha Newcastle.
LIVERPOOL itataka angalau pauni Milioni 20 kutokana na mauzo ya Andy Carroll, kiwango ambacho kitakuwa ni mtihani mkubwa kwa Newcastle kutoa ili kumsajili tena mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England kabla ya msimu mpya wa Ligi Kuu.
KLABU ya Sheffield Wednesday inajiandaa na Ligi Daraja la Kwanza England, maarufu kama Championship kwa kujenga kikosi imara na sasa inapambana na wapinzani, Blackburn na Nottingham Forest kuwani saini ya nyota aliyechokwa QPR, Joey Barton anayetolewa kwa mkopo.
KLABU za Lille na Marseille zina matumaini ya kumnasa mshambuliaji wa Tottenham, Louis Saha, mwenye umri wa miaka 33, arejee Ufaransa kama mchezaji huru.
KIUNGO wa Argentina, Claudio Yacob, mwenye umri wa miaka 24, ambaye awali alikuwa anahusishwa na mpango wa kuhamia Manchester United na Arsenal, anatarajiwa kwenda West Brom, baada ya mkataba wake kumalizika Racing Club ya Buenos Aires.
KLABU ya Manchester City hadi sasa ndio klabu iliyo tayari kutoa ada kubwa ya uhamisho na mshahara mnono kwa Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 28, ambaye amekwishatangaza hatasaini mkataba mpya.
KLABU ya Blackburn ina matumaini ya kumaliza dili la pauni Milioni 2.5 kumsajili mshambuliaji wa West Brom, Simon Cox, 25.
CAPELLO AULA URUSI
MIEZI minne baada ya kubwaga manyanga katika kazi iloiyokuwa inamuingizia pauni Milioni 5 kwa mwaka ya ukocha wa timu ya taifa ya England, kocha Mtaliano, Fabio Capello amerejea kwenye chati, baada ya kuteuliwa kuwa kocha mpya wa Urusi.
URAIA KUMUONDOA MAKOUN ENGLAND
KLABU ya Aston Villa inaweza kumuuza Jean Makoun, mwenye umri wa miaka 29, kwa sababu kiungo huyo wa Cameroon kukosa uraia wa England kunaweza kumsababishia kukosa hati mpya ya kufanya kazi nchini humo.
0 comments:
Post a Comment