Tetesi za J'mosi magazeti ya Ulaya


MAN UNITED WAJIPANGA KUTOA PAUNI MILIONI 30 KUMNASA VAN PERSIE 

KLABU ya Manchester United inahofia mshambuliaji wa Arsenal, Robin Van Persie, mwenye umri wa miaka 28, atawagharimu pauni Milioni 30 katika vita ya Fergie kupambana na wapinzani wao, Man City na Juventus kuwania sani ya nyota huyo wa mabao.
Arsenal striker Robin Van Persie
Van Persie amemkataa kusaini mkataba mpya Arsenal
KOCHA Sir Alex Ferguson anataka kutoa pauni Milioni 8 ili kuinasa saini ya beki wa Everton, Leighton Baines, baada ya kocha huyo wa Manchester United kuthibitisha mpango wa kusajili beki mpya wa kushoto.
Manchester United lazima ilipe kidogo zaidi ili kumpata Lucas Moura, mwenye umri wa miaka 19, kutokana na Sao Paulo kuthibitisha kumuuza kwa pauni Milioni 29.
KLABU ya Galatasaray imesema ipo kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Manchester United, Dimitar Berbatov, mwenye umri wa miaka 31.
MCHEZAJI wa zamani wa Leeds na Liverpool, Harry Kewell, mwenye umri wa miaka 33, ameonyesha nia ya kurejea England baada ya kubwaga manyanga katika klabu ya  Australia, Melbourne Victory.
NYOTA wa Inter Milan, Wesley Sneijder, mwenye umri wa miaka 28, amekataa ofa ya klabu za England, Urusi na Uturuki ili abaki na vigogo hao wa Serie A.
MSHAMBULIAJI aliye kwenye wakati mgumu Manchester City, Roque Santa Cruz, mwenye umri wa miaka 30, anataka kubaki Kaskazini Mashariki, wakati akiangalia klabu nyingine ya kuhamia.
Cheick Tiote
Kiungo wa Newcastle, Tiote anataka kubaki
West Brom imekataa ofa ya pauni Milioni 4 ya kumuuza mshambuliaji, Peter Odemwingie, mwenye umri wa miaka 31, kutoka Al-Gharafa ya Qatar.
Norwich City imeongeza dau ili kumnasa Nahodha wa Leeds, Robert Snodgrass, mwenye umri wa miaka 24, wakati ikipigania kumuunganisha tena kiungo huyo na Bradley Johnson na Jonny Howson.

TIOTE AKATAA OFA YA MAN UTD

KIUNGO wa Newcastle, Cheick Tiote, mwenye umri wa miaka 26, amesema hataondoka The Magpies sasa hivi, licha ya kutakiwa na klabu za kadhaa, ikiwemo Manchester United.
KOCHA wa Chelsea, Roberto Di Matteo ameiambia klabu yake isahau kuwa Mfalme wa Ulaya na kusema kwamba sasa anafikiria namna ya kuwabwaga mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester City.