Tetesi za J'tano magazeti ya Ulaya


SPURS WAMPA 'HELA CHAFU' AVB KUFANYA USAJILI WA KUTISHA

KLABU ya AC Milan imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, Andy Carroll. Pier Silvio Berlusconi, mtoto wa mmiliki wa Milan, Silvio Berlusconi, amekuwa akifanya kazi kama Mshauri wa masuala ya usajili katika klabu hiyo ya Italia na amemtambulisha Carroll kama chaguo sahihi la kusaini.
KLABU ya Everton ipo karibu kumsaini Oscar Cardozo, baada ya Benfica kusema inataka pauni Milioni 16 kumuuza mshambuliaji huyo, ambaye anawaniwa pia na Fenerbahce, Galatasaray, PSG na nyingine kadhaa za Ligi Kuu zinamtolea 'udenda' nyota huyo wa Paraguay.
KLABU ya Tottenham iko tayari kumsaidia kocha wake mpya, Andre Villas-Boas katika soko la usajili kwa kumkatia pauni Milioni 50. Kocha Mreno huyo anataka kuwasajili mshambuliaji wa Marseille, Loic Remy, beki wa Ajax na Ubelgiji, Jan Vertonghen, kiungo wa Hoffenheim, Gylfi Sigurdsson, kiungo wa CSKA Moscow na Urusi, Alan Dzagoev na kipa wa Birmingham, Jack Butland watue White Hart Lane.
KOCHA Andre Villas-Boas anataka aanze kazi Tottenham kwa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Brazil, Oscar kutoka Internacional. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anapatikana kwa dau la pauni Milioni 20.
Andre Villas-Boas
Villas-Boas anaweza kupewa bajeti nzuri ya usajili Spurs
KLABU za Sunderland, Stoke na Fulham zinataka kumsajili nyota wa Wolves, Steven Fletcher lakini klabu hiyo ya Midlands imeonya klabu yoyote inayomtaka mshambuliaji wao huyo iandae pauni Milioni 10.
KOCHA wa Everton, David Moyes anataka kumsajili mshambuliaji aliyemaliza mkataba wake katika klabu ya Wigan, Hugo Rodallega.
KLABU ya Napoli ya Italia, inatazamiwa kukaza msuli katika mbio zake za kuwania saini ya kiungo wa Chelsea, Raul Meireles  baada ya kufanya mazungumzo na wakala wake.
KLABU ya Chelsea ipo karibu kumnasa beki wa pembeni mwenye thamani ya pauni Milioni 6 kutoka Inter Milan, Maicon, na wakala wa Mbrazil huyo atatua London wiki hii kwa mazungumzo.
KLABU za Manchester United na Chelsea zinaingia kwenye vita kali ya kuwania saini ya kiungo wa kimafaifa wa Ubelgiji, Axel Witsel baada ya Benfica kusema wako tayari kumuuza.
KLABU za Malaga na Galatasary zinamtaka mshambuliaji wa Arsenal, Nicklas Bendtner wakati nyota huyo wa Denmark akiwa karibu kuondoka Emirates. Wakala wa Bendtne, Jesper Lynghus ameliambia gazeti moja la Denmark, bold.dk mwezi uliopita kwamba: "maombi ni mengi, itategemea na jinsi Nicklas atakavyocheza Euro 2012."

OTHER GOSSIP

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amevunja ukimya wake juu ya mustakabali wa Nahodha wake, kwa kusema kwamba atambakiza kwa gharama zozote. Wawili hao walitarajiwa kuzungumza kwa simu wakati van Persie akiendelea kuisstiza mkataba mpya wa miaka mitatu na mshahara wa pauni 130,000- kwa wiki.
Robin van Persie (left) and Arsene Wenger (right)
Van Persie na Wenger watakuwa mazungumzo wiki hii
KOCHA wa Arsenal pia amekataa ofa ya kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, kufuatia kujiuzulu kwa Laurent Blanc.
KOCHA Brendan Rodgers anataka mshambuliaji Luis Suarez asaini mkataba mpya wa kuendelea kukipiga Anfield, licha ya tetesi zilizougubika mustakabali wa mshambuliaji huyo. Rodgers amesema kwamba Suarez, ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2016, anafurahia maisha Anfield licha ya tetesi kwamba, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaweza kwenda kwa mabingwa wa Serie A, Juventus.
AND FINALLY... 
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea, Nicolas Anelka amekumbana na kasheshe baada ya shabiki wa Shanghai Shenhua ya China, kumvaa na kumponda kwamba anacheza ovyo.