Tetesi za J'pili magazeti ya Ulaya
MAN UNITED JIANDAENI KUMPOKEA VAN PERSIE
Robin van Persie ametakiwa kutokwenda ziara ya kujiandaa na msimu mpya ya Arsenal na Arsene Wenger - na Manchester United sasa imekuwa klabu iliyo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumtwaa Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 28.
DILI la Manchester United kumsajili Van Persie linayumba kutokana na Arsenal kugoma kupunguza bei kutoka pauni Milioni 30.
Nicklas Bendtner anajiandaa kuondoka Arsenal wiki hii, na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Denmark, mwenye umri wa miaka 24 anatakiwa kwa dau la pauni Milioni 7.5 na AC Milan na Galatasaray.
KINDA wa Barcelona, Gerard Deulofeu, mwenye umri wa miaka 18, yupo kwenye rada za Liverpool na QPR.
Ryo Miyaichi, mwenye umri wa miaka 19, anaweza kuwa na ndoto za kuchezea Arsenal sasa, baada ya kocha wa Ajax, Frank de Boer kuonyesha nia ya kumuachia.
Everton inataka kumsajili kiungo wa kimataifa wa Afrika Kusini, Steven Pienaar, mwenye umri wa miaka 30, kutoka klabu ya Tottenham Hotspur.
KOCHA Michael Laudrup amesema hatasimama upande wa Joe Allen, mwenye umri wa miaka 22, na mchezaji huyo bora aondoke Swansea.
KLABU ya QPR inakusanya pauni Milioni 6 kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Celtic, Mkorea Kusini, Ki Sung-Yeung, 23.
LUCAS LEIVA ALETEA RAHA LIVERPOOL
YUKO fiti tena. Kiungo wa Liverpool, Lucas Leiva ameleta faraja kwenye kikosi cha Brendan Rodgers pale Anfield, kufuatia kupona kwa Mbrazil huyo maumivu ya goti.
MCHEZAJI aliyesainiwa kwa bei chafu Liverpool, pauni Milioni 35, Andy Carroll ataungana na wachezaji wenzake katika ziara ya kujiandaa ns msimu mpya nchini Marekani kesho, licha ya utata uliougubika mustakabali wake.
ROBINHO HAPENDI MAZOEZI...
NYOTA wa AC Milan, Robinho na Kevin-Prince Boateng hawapendi sana mazoezi na zaidi wamekuwa wakijirusha disko kuliko kujifua kwenye Uwanja wa soka.
0 comments:
Post a Comment