Tetesi za J'tatu magazeti ya Ulaya
MAN CITY WATAKA KUIPIGA BAO BAYA ARSENAL
KLABU ya Manchester City inajiandaa kuwapiku wapinzani wao katika Ligi Kuu, Arsenal na Tottenham katika kuwania saini ya kinda mshambuliaji wa Kifaransa, M'Baye Niang, ambaye anachezea Caen.
KLABU ya Chelsea inaweza kupigwa bao katika kuwania saini ya beki wa kulia wa Inter Milan, Maicon na mabingwa wa Hispania, Real Madrid.
MPANGO wa klabu ya Stoke kumsajili kiungo wa kimataifa wa Marekani na klabu ya Houston Dynamos, Geoff Cameron unaweza kufa kutokana na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Marekani, kutaka dau la uhamsho wa mkopo la pauni Milioni 2.2 kwa ajili ya mchezaji huyo.
KIUNGO wa Chelsea, Florent Malouda anaweza kuhamia Santos ya Brazil, baada ya dai lake la nyongeza ya mshahara Stamford Bridge kuonekana kama kupuuzwa hivi.
KLABU za Everton, West Ham na QPR zinakabana koo kuwania saini ya kinda wa miaka 19, mshambuliaji wa Inter Milan, Luc Castaignos.
ANDERSON APANIA MAKUBWA MSIMU UJAO
KIUNGO wa Manchester United, Anderson anataka kuutumia msimu ujao kuthibitisha kwamba yeye ni kifaa na ndiyo maana klabu hiyo ya Old Trafford ilitoa fedha kumnunua kutoka Porto kwa dau la pauni Milioni 25.
0 comments:
Post a Comment