Tetesi za Jumatano magazeti ya Ulaya


MAN CITY YAMNG'OA HIGUAIN REAL MADRID, BARCELONA NAYO YAMTAKA ALEX SONG WA ARSENAL

KLABU ya Manchester City inataka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 24, Muargentina, Gonzalo Higuain.
SITAKI nataka zimeendelea kwa Kibibi Kizee cha Turin. Juventus imesema tena imepoteza dhamira ya kumnunua mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 28.
MSHAMBULIAJI Andy Carroll anataka kuondoka Liverpool tu kurejea klabu yake ya zamani, Newcastle United.
Lakini pia, Tottenham inaelezwa kujipanga kumsajili Carroll, mwenye umri wa miaka 23.
KLABU ya West Ham inataka kumsajili tena beki wa Aston Villa, James Collins baada ya kusitisha mpango wa kumsajili Ivan Ramis, ambaye anaweza kuhamia Wigan.
Alex Song
Alex Song anatakiwa na Barcelona.
Tottenham inataka kumsajili kipa wa Inter Milan, Mbrazil, Julio Cesar, mwenye umri wa miaka 32, baada ya kumkosa Hugo Lloris wa Lyon.
DAU la Sunderland la pauni Milioni 10 kwa ajili ya mshambuliaji wa Wolves, Steven Fletcher, mwenye umri wa miaka 25, limepigwa chini na klabu hiyo ya Daraja la kwanza.
KLABU ya Barcelona imepanga kukata dau la pauni Milioni 11.7 kumsajili kiungo mkabaji wa Arsenal, Mcameroon Alex Song mwenye umri wa miaka 24.
KLABU ya Real Madrid ni kama imeamua kuachana na kiungo wa Tottenham, Luka Modric na sasa inataka kumsajili Mholanzi Wesley Sneijder wa Inter Milan.
KLABU ya Manchester City imemuambia mshambuliaji wake, Emmanuel Adebayor inataka kumuuza moja kwa moja, Tottenham anakocheza kwa mkopo ili kujivuan mzigo wake wa kumlipa.
KLABU ya Stoke City ipo kwenye mazungumzo na Aston Villa juu ya beki Alan Hutton, mwenye umri wa miaka 27, ahamie Uwanja wa Britannia, baada ya kupiga kazi Villa Park kwa miezi 12.

WAKALA AMTETEA CHARLIE ADAM

Mick McCarthy
Mick McCarthy anataka kupiga kazi Ligi Kuu tena.
WAKALA wa Charlie Adam, amemtetea kiungo huyo wa Liverpool kwa rafu aliyochezea winga wa Tottenham, Gareth Bale.
KOCHA wa zamani wa Wolves, Mick McCarthy amesema kwamba amekataa kuwa kocha wa  Nottingham Forest kwa sababu ana matumaini ya kurejea Ligi Kuu.
KLABU ya Portsmouth wanatumai kwamba mpango wa Balram Chainrai kuinunua klabu hiyo kwa mara ya pili utakamilika ndani ya siku kadhaa zijazo.