Tetesi za Jumatatu magazeti ya Ulaya
MAN CITY 'DIZAINI' WAMEMPOTEZEA VAN PERSIE
KLABU ya Tottenham inajiandaa kumsajili nyota wa CSKA Moscow, mwanasoka wa kimataifa wa Urusi, Alan Dzagoev, kwa mujibu wa baba yake.
KLABU ya Wigan imezionya Liverpool na Chelsea kwamba wanataka angalau pauni Milioni 12 kwa ajili ya Victor Moses, mwenye umri wa miaka 21.
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amepunguza kasi ya kumfukuzia mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie.
MSHAMBULIAJI wa Croatia, Danijel Pranjic, mwenye umri wa miaka 31, amesema itakuwa heshima kubwa kwake kujiunga na Everton, baada ya kuondoka Bayern Munich kama mchezaji huru.
KIPA wa Lyon, Hugo Lloris anapatikana kwa bei mwafaka, kwa mujibu wa rais wa klabu yake, Jean-Michel Aulas - na hiyo inazifanya Arsenal, Tottenham na Liverpool zinazomuwania zianze harakati za kuwania saini yake.
EURO 2012
KOCHA Arsene Wenger amekataa ofa ya kuondoka Arsenal kwenda kuchukua nafasi ya Laurent Blanc kama kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa.
MSHAMBULIAJI wa Italia, Mario Balotelli staili yake ya kushangilia bao kifua wazi imeigwa na mshambuliaji mmoja Japan.
AVB NI WHITE HART LANE TU
KIUNGO wa zamani wa Tottenham, Graham Roberts amesema kwamba Andre Villas-Boas hataingia chumba chochote cha kubadilishia nguo, labda cha White Hart Lane.
MSHAMBULIAJI wa Bolton, Marvin Sordell ameitwa 'kizali zali' katika kikosi cha timu ya Uingereza cha kocha Stuart Pearce kitakachoshiriki michuano ya Olimpiki.
KIUNGO Adam Johnson atahakikishiwa mustakabali wake katika klabu yake ya Manchester City mara atakapofanya mazungumzo na kocha Roberto Mancini wiki hii.
0 comments:
Post a Comment